,

,

Saturday, 14 December 2013

MTAYARISHAJI WA VIDEO ZA MUZIKI NISHER ATOA OFA ZA MSIMU WA SIKUKUU, HICHI NDICHO ALICHOPOST KWA FACEBOOK

Umeshafanya Booking yako ya Music video kwaajili ya kushoot January? Kama bado fanya sasa, offer ya siku kuu kwa video moja ni Tsh 1, 000, 000 tu badala M-3... video zote zitakazo lipiwa kuanzia dakika hii zitafanyika January. offer inaisha mda wowote, Wahi mapema!! -nisher +255785959599
Like · · · 2 hours ago ·

Wednesday, 11 December 2013

''NILIMTUNGIA MATONYA NYIMBO YA VAILETI NA DUNIA MAPITO LAKINI HANA SHUKRANI''..TUNDA MAN

Msanii wa muziki wa kizazi kipya Tunda Man hivi karibu alizungumzia kwa namna alivyokuwa akimtungia nyimbo msanii wenzake wa muziki huo aitwa Matonya na fadhila alizozipata.

http://dartalk.com/wp-content/uploads/2013/01/tundaman.jpg
Akizungumza kwenye kipindi cha The Takeover kinachorushwa na kituo cha TBC fm, Tunda Man alisema, yeye ndiye ambaye alitunga na kuandika nyimbo mbili zilizompa jina Matonya, yaani Vaileth na Dunia mapito, "mimi ndiye ambaye nilitunga na kumuandikia Matonya zile nyimbo, yaani ule wa Vaileth na Dunia mapito". Alisema Tunda Man a.k.a Captain Tunda.

"Unajua ni hivi, Vaileth ni jina la dada yangu na nililitumia jina lile kwa sababu hiyo, nilimtungia na kumpa kama mshikaji ila kwa sasa siwezi kufanya hivyo kwa sasa sababu Matonya hana shukurani, japo juzi kati aliniomba nimtungie wimbo".

"Unajua binadamu tunatofautiana, hebu fikiria jamaa alishindwa japo kurudisha fadhila hata kwa mama yangu mzazi ambaye kwa kipindi kile alikuwa anatusaidia mimi na mshkaji japo kwa hela ndogo ndogo kama nauli nk. ila baada ya kutoka yote hayo aliyasahau na kuendelea na maisha yake, kweli tenda wema uende zako," alisema Tunda Man huku akiendelea. "Hii wala sio siri na muulize hata yeye na kama atabisha niambie".

Mtangazaji wa kipindi Dan Chibo alipomuuliza kwa nini hukuziimba wewe mwenyewe, Tunda Man alijibu, " kwa kipindi kile mimi nilikuwa siimbi sababu nilikuwa siamini kama kwa sauti yangu ningeweza kuwa ni muimbaji, niliamua kumtungia yeye kwa sababu hiyo". 

Aliendelea kwa kusema "Siku moja nilikutana na mtaalamu mmoja kule Bagamoyo kwenye Chuo cha Sanaa na kunieleza kwamba sauti niliyo nayo ni sauti nzuri na inafaa kwa kuimba, na nikifanya hivyo nitakuja kuwa mwanamuziki mkubwa mwenye sauti ya kipekee, jamaa sitomsahau sababu yeye ndiye aliyenifungua kwenye hili, namshukuru sana".


Tuesday, 10 December 2013

Mwonekano wa Mabasi Mapya yaendayo Kasi Jijini Dar, Mwonekano wa Nje na Ndani..!





Mabasi ya mwendo kasi 2014 kimara kivukoni.  Picha kwa hisani ya Deo Mutta Mwanatanga 

Huu ndio Mjengo wa Msanii SHILOLE..!!

Wakati ambapo Shilole anaendelea kumuomba Mungu amalizie mjengo wake uliopo Kimara jijini Dar es Salaam, Fid Q anaonesha kuzungusha mkwanja alionao kwenye biashara ya madini.
Shilole amepost Instagram picha ya nyumba yake iliyopo kwenye hatua ya mwisho kukamilika na kuandika: Mungu nisaidie nimalizie hii kitu ili watoto wangu wasije kupata tabu.”



Naye Fid Q amepost picha inayoonesha madini ya ruby na kuandika: #RubySozite #NewHustle roll a phat 1 fi ya Nig..!!!”

Usiyoyajua kuhusu MWAMVITA MAKAMBA...Binti wa Mzee Yusuph Makamba mwenye Mafanikio na mfano wa Kuigwa...!!

theclicktz.com/

theclicktz.com/

theclicktz.com/

theclicktz.com/

Mwamvita Makamba, Ni mtoto wa Muheshima Makamba aliyekuwa mkuu wa Mkoa Wa Dar es salaam , na baadae Mwenyekiti wa CCM kitaifa, Mwamvita ana Masters ya  Politics and International Relations na kwasasa ni Chief Officer: Marketing & Corporate Affairs kampuni ya Vodacom Tanzania. 
Tujifunze kwa huyu dada..

Sista duu Anusurika kubakwa hadharani mara baada ya Kukatisha na Kimini kinachoonyesha Nyeti zake huko Kariakoo..!!


MREMBO wa haja ambaye jina halikupatikana amenusurika kubakwa na wanaume baada ya kuvaa kivazi kilichoacha wazi sehemu kubwa ya maungo yake nyeti.

Mrembo aliyevaa kivazi cha ajabu kilichoacha wazi sehemu zake nyeti akisaidiwa na wasamaria wema baada ya kuvaa khanga.




Mrembo huyo akizongwa na vijana wa Kariakoo.
Tukio hilo lilijiri sehemu yenye mkusanyiko mkubwa, Kariakoo jijini Dar ambapo mrembo huyo alikuwa kwenye ‘shopping’ kwa ajili ya sikukuu ijayo ya Krismasi.


Akisaidiwa kuingia kwenye gari.
Likiwa linarandaranda maeneo hayo, Ijumaa Wikienda lilinasa laivu tukio hilo ambapo mrembo huyo alivuliwa nguo hadharani na kuacha ‘vitu’ njenje vikishuhudiwa hata na watoto waliokuwa wakimzomea.

Wanaume hao waliokuwa wakiongezeka na kuanza kumshika sehemu nyeti, walisababisha dada huyo kuanza kutoka nduki ambapo alizama kwenye duka moja kisha akasitiriwa kwa khanga na mama mmoja msamaria mwema.


Akiwa ndani ya gari.
Alipotoka bado wanaume waliendelea kumzingira ambapo ilimlazimu kutoa shilingi elfu hamsini kisha kurukia kwenye ‘kenta’ iliyomuondoa eneo hilo na haikujulikana alikoelekea kwa sababu gari hilo lilichomoka mbio huku akiwa amekoma ubishi wa kutembea nusu utupu.


Vijana wakilizonga gari alilopanda mrembo huo.

Dk. Slaa Kuunguruma Jimboni kwa Zitto kabwe Leo...!!

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Wilbrod Slaa leo atakuwa na ziara ya siku moja katika Jimbo la Kigoma Kaskazini ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake ya siku tisa mkoani Kigoma kwa ajili ya kuimarisha chama.
 

Jana jioni, Dk Slaa alifanya mkutano wa hadhara Mjini Manyovu na kusema kuwa hatishwi na waandamanaji wala vitisho vya kuuawa na kusisitiza kuwa ataendelea na ziara yake kama kawaida hadi Kigoma Mjini.
 
Awali, akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Malumba wilayani Kasulu, juzi Dk Slaa alisema siyo mara yake ya kwanza kutishwa na kusema analindwa na Mungu.
Licha ya kukabiliwa na upinzani kutoka kwa baadhi ya wanachama wanaodai kupinga hatua ya Kamati Kuu kumvua nyadhifa zake zote, aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wake, Zitto Kabwe alisema ataendeleza kazi kuimarisha uhai wa chama kama ratiba ilivyopangwa.
Akiwa katika jimbo hilo linaloongozwa na Zitto, Dk Slaa atatembelea Vijiji vya Nyarubanda na Kidahwe na kufanya mikutano ya hadhara inayosubiriwa kwa hamu na wadau wa siasa nchini kutokana na mzozo huo uliokikumba chama hicho kikuu cha upinzani nchini.
Mwenyekiti wa Chadema Jimbo la Kigoma Kaskazini, Ally Kisala alisema maandalizi ya mikutano hiyo yamekamilika na kwamba hakuna hofu yoyote ya kutokea vurugu katika mikutano hiyo.
Tumedhibiti aina yoyote ya vurugu iliyokusudiwa licha ya kuwapo baadhi ya watu wanaotamani hayo yatokee kwa lengo lao binafsi, sambamba na kunufaisha masilahi ya makundi binafsi, lakini hayatatokea,” alisema.
Juzi, wanachama na wafuasi wa Chadema wanaomuunga mkono Zitto waliandamana kupinga ziara ya Dk Slaa katika jimbo lao kupinga hatua ya kumvua mbunge wao madakara.
“Tunaamini mikutano yote ya kesho (leo Jumanne) itafanyika vizuri na watu watapata ujumbe kutoka kwa Katibu Mkuu wetu (Dk Slaa), na pengine wale wanaopiga kelele na kutaka kuleta mgawanyiko ndani ya chama watapata fursa ya kuujua ukweli wa mambo ndani ya chama.
Vita yetu si kukigawa chama, bali ni kuhakikisha tunaingia Ikulu katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015,” alisema Kisala.
Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Zedekia Makunja alisema jeshi lake limejipanga kuhakikisha usalama unakuwapo katika ziara hiyo.
Tunawajibika kuhakikisha usalama unakuwa vizuri na kila jambo linaendelea kama lilivyopangwa. Mwito wangu kwa viongozi, wanachama na wapenzi wa Chadema ni kuhakikisha wanamaliza tofauti zao mapema ili kuepusha madhara yanayoweza kujitokeza, hatupendi kuona askari wetu wakilazimishwa kutumia nguvu kudhibiti hali ya usalama,” alisema Makunja

Wanahitajika waimbaji chipukizi wa muziki wa Injili Tanzania, Changamkia Fursa.

Huduma Ya UPENDO & FURAHA ya jijini Dar es salaam, inatafuta vijana wa Kikristo wali okoka, kwa ajili ya kuunda kwaya ya muziki wa injili itakayokuwa ikihudumu katika mikoa mbalimbali ya Tanzania na katika nchi jirani.

SIFA ZA WATU WANAOHITAJIKA:-

i. Awe na karama ya uimbaji.
ii. Awe na umri wa kuanzia miaka 16 hadi 35.
iii. Awe ameokoka na mwenye hofu kuu ya Mungu.
iv. Awe na wito wa kweli wa kumtangaza na kumtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji.
v. Awe na utayari, pamoja na muda wa kutosha wa kusafiri na huduma katika mikoa mbalimbali ya Tanzania pamoja na nchi jirani.
vi. Awe mkazi wa Dar es Salaam.

Usaili utafanyika siku ya tarehe 06 Januari 2014.

MWISHO wa kujiandikisha ni tarehe 24 Desemba 2013.

Ili kujiandikisha, fikaofisini kwetu siku za kazi kuanzia saa tatu kamili asubuhi hadi saa kumi kamili jioni, au wasiliana nasi kwa namba ya simu 0784406508.

Msanii wa Hip pop 'THE GAME' kuchora tattoo ya MANDELA mwilini mwake..!!

Rapper kutoka pande za Marekani The Game ameonyesha jinsi anavyompenda Nelson Mandela kwa kujichora tattoo ili kumuenzi Nelson Mandela. Kupitia mtandao wake wa instagram, The Game alisema



“The finished ‘Nelson Mandela lookin out of the prison bars by @NikkoHurtado done on my side. 7 hour sitting…. Few more hours to tie in the tats around it & we solid. 


#NelsonMandela #RIP #Legend #Leader #Freedom #Peace #Equality #Tattoos #SouthAfrica

Roy Keane amponda Ferguson na Kudai kuwa ana tamaa ya Madaraka makubwa ndio maana Man utd inaboronga...!!

Nahodha wa zamani wa Manchester United, Roy Keane amesema kwamba kocha aliyeng’atuka katika klabu hiyo, Sir Alex Ferguson bado ana uchu wa madaraka. Keane aliyeondoka baada ya kukosana na klabu hiyo na pia amekuwa akitupiana maneno na Fergie amedai kwamba Ferguson anatafuta nguvu za kimadaraka na kimamlaka ili adhibiti mambo Old Trafford. Fergie alistaafu Mei mwaka huu na kumpendekeza raia mwenzake wa Scotland, David Moyes aliyekuwa Everton kuchukua nafasi yake, huku Fergie akiingia kwenye bodi kama mkurugenzi. Tangu hapo Manchester United wamefanya vibaya kwenye ligi, ambapo sasa wanashika nafasi ya tisa baada ya kupoteza mechi tano, jambo ambalo si kawaida kwao. “Kila kitu hapo 



Ferguson anafanya kwa ajili ya udhibiti na mamlaka,” anasema Keane aliyecheza hapo chini ya Ferguson tangu 1993 hadi 2005 akacheza mechi 326 kama mmoja wa viungo bora zaidi na akafunga mabao 33. “Bado anapigania kupata mamlaka hadi sasa hivi ili awe na sauti kwenye timu japokuwa sio kocha tena – kuna ubinafsi mkubwa sana unaohusishwa hapa,” anasema Keane. Mchezaji huyo wa zamani na mchambuzi wa masuala ya soka kwa sasa ni kocha msaidizi wa Timu ya Taifa ya Jamhuri ya Ireland na anasema hawana tena uhusiano hata kidogo na Fergie.

"Tulimwondolea MANDELA mashine za kupumulia akafariki masaa mawili baadae"...Madaktari

Rafiki wa karibu wa familia ya Nelson Mandela, Bantu Holomisa amesema madaktari walikata tamaa kiongozi huyo na kumwondolea mashine ya kupumulia na kufariki dunia baada ya saa mbili. 
 

Alionekana ametulia kana kwamba amelala na hiyo ilionyesha kuwa madaktari walikuwa wameshakata tamaa na wamefikia mwisho wa kupigania maisha yake,” alisema Holomisa na kukaririwa na Shirika la Habari la AP.
Rafiki huyo wa Mandela ambaye alikuwa na familia hiyo kabla na baada ya Mandela kutoka gerezani mwaka 1990, aliiambia AP kwamba aliitwa na wanafamilia hasa baada ya hali ya Mandela kubadilika na kuwa mbaya zaidi.
Holomisa alisema alipofika nyumbani, alikuta wanandugu 20 wamekusanyika wakiwa wamemzunguka. “Niliona watu wakiwa wanahangaika naye na nilijua tu kuwa sasa imefikia hatua ya mwisho... baada ya saa mbili, Mandela alifariki dunia.

Monday, 9 December 2013

HISORIA YA MAISHA YA NELSON MANDELA KWA UFUPI

Miaka ya Mapema
African National Congress president Nelson Mandela
 1952
Rolihlahla Mandela, mwanawe chifu, alizaliwa katika kijiji kimoja kiitwacho, Mvezo katika mkoa wa Eastern Cape nchini Afrika Kusini tarehe 18 Julai mwaka 1918. Alikuwa mtu wa kwanza katika familia yake kwenda shule. Mwalimu ambaye hata hangeweza kutaja jina lake vyema, alizoea kumuita Nelson. Alitoroka mjini Johannesburg mwaka 1941 ili kuepuka kulazimishwa kuoa mapema. Alikutana na Walter Sisulu aliyemsaidia kupata kazi katika kampuni ya ya Witkin Sidelsky na Eidelma. Pia alijiunga na chama cha (ANC)
Kesi ya Uhaini
1956
Mandela alifuzu kama wakili na kuanzisha kampuni ya kwanza ya sheria inayomilikiwa na mtu mweusi mwaka 1952 na kuiendesha kwa ushirikiano na Oliver Tambo, na kutoa huduma za kisheria kwa wale ambao walikosa uwakilishi. Akihofiwa kupigwa marufuku na serikali ya ubaguzi wa rangi, ANC ilimtaka Mandela kuhakikisha kuwa chama hicho kinaweza kuendesha harakati zake kimya kimya. Alikamatwa mwaka 1956 na kufunguliwa mashtaka ya uhaini yeye pamoja na wenzake 155. Baada ya kesi yake iliyochukua miaka minne, ilitupiliwa mbali . Mnamo mwaka 1958, Mandela alimuoa Winnie Madikizela.
Kufungwa Maisha
1964
Sheria ya hali ya hatari ilitangazwa baada ya polisi kuwaua waandamanaji 69 mjini Sharpville mwaka 1960. Serikali ilihofia kuwa wangelipiza kisasi na hivyo kuharamisha chama cha ANC. Chama hicho baadaye kiliendesha harakati zake za kijeshi kichinichini wakiongozwa na Mandela.Mwaka 1962, Mandela alikamatwa kwa kosa la kuondoka nchini bila kibali. Wanachama wengine wa ANC walikamatwa. Akiwa jela Mandela alishtakiwa kwa kosa la hujuma. Yeye na wengine saba walihukumiwa jela katika kisiwa cha Robben mwaka 1964
Huru hatimaye
1990
Jamii ya kimataifa iliiwekea vikwazo zaidi serikali ya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini. Vikwazo vya kwanza viliwekwa mwaka 1967.Shinikizo zilizaa matunda na mnamo mwaka 1990, rais FW De Klerk akakiondolea marufuku chama cha ANC. Tarehe 11 Februari, Mandela aliachiliwa baada ya miaka 27 jela. Umati wa watu ulimshangilia huku yeye pamoja na mkewe wakiondoka sehemu ya jela. Katika mkutano wa kwanza wa chama cha ANC mwaka uliofuata, Mandela alichaguliwa kama kiongozi wa chama .Mazungumzo yakaanza ya kuunda serikali ya pamoja ya waafrika weusi na wazungu.
Tuzo ya amani ya Nobel
1993
Mnamo mwaka 1993, Mandela na rais wa nchi hiyo wakati huo, walituzwa tuzo ya amani ya Nobel kwa juhudi za kuleta uthabiti Afrika Kusini. Akikubali tuzo hiyo, Mandela alisema kuwa ” tutafanya kila tuwezalo kuweza kuleta mageuzi duniani.”
Rais mpya
1994
Mnamo mwaka1994,kwa mara ya kwanza katika historia ya Afrika Kusini, watu wa rangi zote walipiga kura katika uchaguzi huru na wa kidemokrasia. Mandela alichaguliwa. Akihutubia umma, katika sherehe ya kuapishwa kwake, tarehe 10 mwezi Mei, mwaka 1994, alisema: “uhuru utawale, Mungu aibariki Afrika!” Tatizo lake kubwa lilikuwa ukosefu wa nyumba za kutosha kwa watu maskini na mitaa ya mabanda iliendelea kuongezeka.Thabo Mbeki alichukua uongozi wa nchi huku Mandela akiuza sera za nchi hiyo kimataifa.
Akitoka Robbben
1995
Kuadhimisha miaka mitano baada ya kuachiliwa kwake, Nelson Mandela alizuru kisiwa cha Robben mwezi Februari mwaka 1995 alikozuiliwa kwa miaka 18. Ziara yake ilikuwa mwaka 1956 mwezi Februari pamoja na wafungwa wenzake waliowahi kufungwa kisiwani humo na kufanya kazi ngumu. Mapafu ya Mandela yanasemekana kuathirika alipokuwa anafanya kazi katika machimbo ya mawe.
‘Usiniite”
2004
Thabo Mbeki alichukua mamlaka kutoka kwa Mandela kama kiongozi wa chama tawala ANC na hata kushinda uchaguzi wa mwaka 1999.Mandela alimuoa Graca Machel, mjane wa aliyekuwa rais wa Msumbiji, akiwa na miaka 80. Aligunduliwa kuwa na saratani ya Tezi Kibofu na hivyo kuanza matibabu.Mnamo mwaka 2004, alitangaza kujiuzulu, akisema kuwa anataka maisha ya kimya nyumbani kwake na familia yake. Kwa mzaha aliwaambia wandishi wa habari wasimpigie simu.
Sherehe ya siku ya kuzaliwa kwake
2008
Wanamuziki, waigizaji na wanasiasa waliungana na Mandela katika sherehe kubwa uwanja wa Hyde Park mjini London kusherehekea miaka 90 ya kuzaliwa kwake. Akiongea na wale waliofika, aliwaambia, ”ni wakati kwa kizazi kipya kuchukua uongozi, kibarua kwenu sasa.”
Kuugua
2010
Mandela aliweza kuonekana hadharani mara kadhaa baada ya kustaafu. Ingawa alionekana katika sherehe ya kukamilika kwa dimba la kombe la dunia mwaka 2010 nchini humo. Januari mwaka 2011, alilazwa hospitalini kwa ukaguzi maalum, huku serikali ikiwakumbusha watu kuwa aliwahi kupata matatizo ya kupumua. Alipokea matibabu ya ugonjwa wa mapafu mwaka 2012 na pia mwaka 2013 .
Kufariki
2013
Nelson Mandela anefariki usiku wa kuamkia lea baada ya kuugua kwa muda mrefu maradhi ya mapafu.

CHANGAMOTO INAYOWAKABILI BAADHI YA WANAWAKE WAINGIAPO KATIKA MAHUSIANO MAPYA..


Ni pale mwanaume anapoonyesha tamaa kubwa ya ngono na kulazimisha kukutana kimwili wakati mwanamke aliweka msimamo wa kutokutana kimwili na mwanaume yeyote mpaka baada ya muda fulani tangu kufahamiana na kuwa wachumba au mpaka pale watakapofunga ndoa

Huu ni mtihani kwa wanawake wengi kwa sababu unawaweka katika wakati mgumu wa kuchagua kuvunja nadhiri waliojiwekea au kusimama imara kwenye msimamo waliyojiwekea kwa ajili yakulinda heshima zao.


Swali kwa wanawake: Je unapokabiliwa na mtihani kama huu ni uamuzi gani unaona ni sahihi kwako….?

Hivi Ndivyo Msanii Maarufu Nchini Marekani Kelly Rowland Alivyotembelea Mitaa ya Manzese Uswahilini Jijini Dar...!!

Msanii maarufu wa Marekani Kelly Rowland, ametinga uwanja wa fisi Manzese Dar es salaam jana jioni baada ya kusikia sifa za maeneo hayo ya Uswahilini tangu akiwa USA. Msanii huyo ametua nchini kwa tiketi ya MTV kupitia taasisi yake inayojishughulisha na kampeni za kupambana na Ukwimwi (Staying Alive Foundation) ya nchini Marekani, Kelly akiwa balozi wake. Akiwa Uwanja wa Fisi, ambako kunasifika kwa ufuska wa kupindukia na rate kubwa ya maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa wasichana wadogo, Kelly alitembelea NGO ya EYG (Elizabeth Youth Group) inayojishughulisha na kutoa misaada ya elimu ya HIV/AIDS, uchangudoa, ulevi pamoja na uvutaji bangi kwa vijana nchini.



Picha 7 za vurugu kubwa zilizotokea Kasulu Kigoma Kumpinga Dr. Slaa......Mabango yao yanasema CHADEMA ni mali ya Wachaga.


Baada ya mkutano wa Dr. Slaa Kuvunjwa  kwa fimbo  na mawe, kilichofuata  baadae  ni  mapambano  kati  ya  polisi  na  wananchi  wanaompinga Dr. Slaa 

WOSIA wa MANDELA wazua mjadala mkali..!!

Marehemu Nelson Mandela enzi za uhai wake. Mwandishi Wetu na Mitandao
WOSIA aliowahi kuuandika hayati Nelson Rolihlahla Mandela ‘Mzee Madiba’ au ‘Tata’ (95) enzi za uhai wake akielezea anavyotaka azikwe, ndiyo tishio kubwa lenye utata kuelekea siku ya mazishi yake, Jumapili ijayo, Ijumaa Wikienda limebaini.
Mtandao mmoja nchini humo umeukumbushia wosia huo huku familia ikianza kuonesha misimamo tofautitofauti, hali inayoashiria kuibuka kwa makundi mawili yanayokinzana.



Gari lililobeba mwili wa Nelson Mandela.
FAMILIA INAVYOTAKA
Habari za ndani zilisema kuwa familia inataka mazishi ya kiongozi huyo maarufu duniani yawe makubwa na ya kisasa kwa vile viongozi wa nchi mbalimbali duniani watahudhuria.
“Mandela ni kingozi mkubwa sana duniani, mazishi yake lazima yawe makubwa pia ya kisasa. Hawezi kuzikwa kama mwananchi wa kawaida,” ilisomeka sehemu ya taarifa hiyo.


Mmoja wa waombolezaji akigusa picha na Mandela.
Taarifa hiyo iliongeza kuwa wakati familia hasa wajukuu na watoto wake wakishikilia msimamo huo, wapo wanandugu wanaotaka azikwe kama alivyoandika katika wosia wake huo.
SERIKALI YAPANGA MAMBO BILA KUFUATA WOSIA
Habari zaidi zilisema kuwa Serikali ya Afrika Kusini inajitahidi kuupangua wosia huo kwa kuendelea na maandalizi ya mazishi kama haukuwahi kuwepo licha ya kwamba jamii ya watu nchini humo inaheshimu wosia wa marehemu.

WOSIA UNAVYOSEMA
Mzee Madiba alishauandika wosia huo kwenye karatasi moja tu ambapo aliagiza anavyotaka azikwe. Alisema kuwa akifa azikwe katika milima iliyojitenga nyumbani kwa mababu zake katika Kijiji cha Qunu, Eastern Cape huko ‘Sauzi’.


Waombolezaji wakiweka maua katika sanamu la Mandela.
ALITAKA MAZISHI YA KAWAIDA SANA
Inadaiwa wosia huo aliuandika Januari, 1996 wakati bado akiwa rais ambao ulijaa maelekezo yote juu ya mazishi yake. Aliagiza kufanyiwa mazishi ya kawaida sana yenye hadhi ya raia wa kawaida nchini humo hivyo kuyafanya kuwa makubwa na ya kifahari ni kukiuka wosia wa mzee.

KABURI ALILOLITAKA MANDELA
Katika wosia wake huo uliotolewa na rafiki yake wa karibu, Mzee Madiba aliandika kuwa akifa azikwe katika eneo la familia lenye makaburi ya ukoo wa Mandela kijijini hapo.
Pia aliagiza kuwa kaburi lake liwekewe jiwe la kawaida kama alama ya mahali lilipo ili lisije kupotea kwa mvua au mabadiliko ya tabia nchi.

Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma.
KABURI LISISAKAFIWE
Katika tafsiri ya maneno hayo, Mzee Madiba alitaka kaburi lake liwe la kawaida sana, akimaanisha lisijengewe kama ilivyokuwa kwa makaburi ya viongozi wengine wa mfano wake barani Afrika kama, Mwalimu Julius Nyerere wa Tanzania na Kamuzu Banda (aliyekuwa Rais wa Malawi).

WOSIA WAKE ULIKUWA WA UPANDE MMOJA WA KARATASI
Magazeti ya nchini humo, South African Mail na Guardian miezi ya karibuni yaliripoti kumnukuu rafiki huyo wa siku nyingi wa familia ya Mandela akisema: “Madiba hakuwahi kukifanya kifo kuwa jambo kubwa la kufikiriwa, pia hakuwahi kutaka chochote cha fahari wakati wa kumzika.”
Cha ajabu, wosia huo wa Mandela ulitosha kwenye upande mmoja wa karatasi ya kawaida ya kuandikia licha ya kwamba mauzo ya kitabu chake cha Long Walk to Freedom na michoro yenye jina lake vilimpatia mamilioni ya fedha.


Nelson Mandela (kulia) akiwa na Mwalimu Julius Nyerere enzi za uhai wao.
FAMILIA YACHUKIZWA NA WOSIA
Wosia huo ulielezwa kuwashangaza watu wengi duniani kwani waliamini angekuwa na vitu vingi vya kuandika kulingana na uwezo wake.
Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Afrika Kusini, SABC, suala hilo la sehemu atakayozikwa Mzee Madiba liliiudhi mno familia yake akiwemo yule mjukuu wake ambaye ni chifu, Mandla Mandela aliyewahi kufikishwa kortini kwa kuhamisha makaburi hayo ya ukoo na kuyapeleka sehemu nyingine. Pia ndiye msemaji wa familia ya Mandela.

DUNIA YAMKATALIA
Baadhi ya wanaharakati ulimwenguni kote walisema wosia huo unapingana na matakwa ya dunia nzima, ambapo walitaka maziko ya mzee huyo yawe  makubwa na ya kihistoria ambayo hayajawahi kutokea.Ilifahamika kwamba dunia inataka mazishi hayo yavunje ile rekodi iliyoshikiliwa na mazishi ya Papa John Paul II aliyefariki dunia Aprili 2, 2005.

Mjukuu wa Nelson Mandela, Mandla Mandela.
SAFARI HII HAKUKIMBIZWA HOSPITALI
Mzee Madiba ambaye alitimiza umri wa miaka 95 Julai 18, mwaka huu, alikuwa hospitalini kwa karibu miezi  mitatu nyuma akitibiwa maambukizi kwenye mapafu huku akipumulia mashine. Baadaye alipata nafuu na kurudishwa nyumbani ambako usiku wa kuamkia Ijumaa iliyopita aliugua ghafla na kufariki dunia.