Huduma Ya UPENDO & FURAHA ya jijini Dar es salaam, inatafuta
vijana wa Kikristo wali okoka, kwa ajili ya kuunda kwaya ya muziki wa
injili itakayokuwa ikihudumu katika mikoa mbalimbali ya Tanzania na
katika nchi jirani.
SIFA ZA WATU WANAOHITAJIKA:-
i. Awe na karama ya uimbaji.
ii. Awe na umri wa kuanzia miaka 16 hadi 35.
iii. Awe ameokoka na mwenye hofu kuu ya Mungu.
iv. Awe na wito wa kweli wa kumtangaza na kumtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji.
v. Awe na utayari, pamoja na muda wa kutosha wa kusafiri na huduma katika mikoa mbalimbali ya Tanzania pamoja na nchi jirani.
vi. Awe mkazi wa Dar es Salaam.
Usaili utafanyika siku ya tarehe 06 Januari 2014.
MWISHO wa kujiandikisha ni tarehe 24 Desemba 2013.
Ili kujiandikisha, fikaofisini kwetu siku za kazi kuanzia saa tatu kamili asubuhi hadi saa kumi kamili jioni, au wasiliana nasi kwa namba ya simu 0784406508.
No comments:
Post a Comment