"R.O.M.A Sijajua nyie mnalionaje hili wenzangu... lakini mimi naona kwa asilimia nyingi(siyo wote) ila nyingi!!!
.....ya kuwa vijana wengi tunalilia na kuhangaikia sana ajira..lakini bado hatujakuwa na wito ktk kazi zetu, bado hatujakuwa na busara na hekima ktk ile kazi tunayotaka!! na bado tumekosa maadili katika kazi ile husika tuitakayo!!
Katika vitengo vingi vya kazi hapa nchini, fananisha huduma atakayokupa kijana na huduma atakayokupa mzee wa makamo/ ama mzee kabisa/mtu mzima!!
Ni mara nyingi sana ukienda ktk huduma mbali mbali kama bank/hospital/wizarani/mashuleni/taasisi mbali mbali/kampuni kadha wa kadha/ toka huko njoo hata ktk mahoteli/bar/na sehemu za kawaida n.k..
....then umkute sista du tu binti fresh from school/ama kijana wa kiume(brother tu) pasipo sababu yoyote anaweza akakuletea nyodo/dharau/majigambo yani kukumbwelesha tu ili ujue bila ya yeye huwezi fanikisha jambo lako!!
WANAKOSEA saaana!!!! kivipi sasa mimi nije bank/ama kwenye kampuni yako ya simu kurekebisha line yangu ya simu!! aaaf eti nikunyenyekee saaana niwe muoga kwako na nikubembeleze? wakati wewe ndiyo unatakiwa uninyenyekee na kunibembeleza mimi mteja..maana bila mimi kuleta line yangu hapo wewe hutapata mteja so utakufa njaa wewe!! na bila mimi kuja bank kuweka pesa zangu hapo basi wewe hutapata pesa ktk ofisi yako..sasa pesa zangu aaf still niwe mdogo mbele yako!!?INAHUU!!
Ni tofauti na unapomkuta mzee ktk ofisi fulani, sawa wazee wetu wana mapungufu yao lakini wengi ni wenye busara na hekima kazini...hata majibu yao yanatia moyo na yanakufanya ujisikie wewe ni wa muhimu!! wana uzoefu na kazi zao kwa miaka mingi!!
Sasa sisi vijana tunalilia sana ajira na tunataka sana tuwatoe wazee wetu ktk viti vyao walivyokalia..sawa wanakubali kutupisha...basi tutoe huduma nzuri na inayopaswa!!
aaaf kuna vitu vingine ukifanya wala hupungukiwi na kitu aisee tena sana sana utaongeza urafiki na utapendwa na watu!!
Ukienda kampuni fulani una shida fulani..aisee unaweza ukamkuta mdada akakupa majibu hayo hadi ukajitoa thamani...
sasa nauliza mdada yule hawazi kuwaza kuwa hata mimi nina kazi yangu... na ipo siku anaweza akanikuta hata mimi ni KONDA wa mbagala tandika na yeye akawa kapoteza nauli na mimi nikaanza kumringia na ofisi yangu isiyo na A.C!!!
kila anaekuja ktk ofisi yako siyo hohe hahe jamani kuwa yupo yupo tu hana mchongo..ipo siku nawewe utamkuta ktk kiti chake akikutazama kwenye foleni huku anakupania usogelee meza yake tu uifikie AKUFURAHISHE!!!
VIJANA TUITAFTE AJIRA LAKINI TUNAHITAJI MABADILIKO NA TUPEWE HASA SEMINA ZA MAADILI/BUSARA NA HEKIMA KAZINI!!!
Says Rooomaaa!!!"
,

Friday, 15 November 2013
FAHAMU ALICHOKIZUNGUMZA ROMA KUHUSU AJIRA TANZANIA
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment