,

,

Saturday, 8 November 2014

Mdogo wake na Kim Kardashian, Kendall Jenner anatamani Penzi la Chris Brown, huenda akampiku Karrueche Tran

Mdogo wake na Kim Kardashian, Kendall Jenner anadaiwa kumzimikia Chris Brown.
1415395842516 (1)
Kuanzia Kulia: Trey Songz, Kendall Jenner, Chris Brown na Kyle Jenner
Model huyo mwenye miaka 19, amekuwa akionekana kwenye picha akila bata na staa huyo miezi ya hivi karibuni na anaamini kuupeleka uhusiano wao kwenye hatua ya juu zaidi. Anasemekana kufanya kila awezalo kufanikisha hilo na anadaiwa kuongea naye kwenye simu mara kwa mara.
1415395842516
“Humtumia Chris selfies zake za kuvutia mara kwa mara,” mtu mmoja wa karibu ameliambia jarida la Uingereza, Heat. “Kendall ameoza kwa Chris – anasema anampenda mno Chris. Anasema amekuwa dhaifu kwake na kwamba wametokea kupatana sana.”
Hata hivyo hivyo dada yake, Kim Kardashian anadaiwa kutofurahishwa na anachokisikia. Chris aliwahi kumpiga mpenzi wake wa zamani, Rihanna, amewahi kukaa rehab na jela na kuwa na uhusiano kwa wakati mmoja tena na Rihanna huku akiwa na mpenzi Karrueche Tran.
Kendall anadaiwa kuvutiwa na uhusiano wa Kim na mumewe Kanye West na yeye pia anataka kuwa na boyfriend maarufu.

No comments:

Post a Comment