Msanii
wa kundi la Tip Top Connection Khalid Ramadhan aka Tunda Man, alikuwa
ni miongoni mwa watu waliokuwa wanamiliki silaha za moto (bastola), kitu
kilichofahamika na kuandikwa na baadhi ya vyombo vya habari mapema
mwaka huu.
Tunda amesema
kwa sasa hamiliki tena bastola, sababu aliamua kuisalimisha silaha hiyo
aliyokuwa anamiliki kutokana na masharti mengi ya kuimiliki.
“Mimi
imenishinda mpaka nimerudisha, Kwasababu watu wengi walikuwa wanajua
mimi nilikua na bunduki halafu maneno yakawa mengi”. Alisema Tunda leo
katika kipindi cha XXL cha Clouds FM Tunda amesema kati ya masharti
yaliyomshinda ni pamoja na aina ya mavazi anayotakiwa kuyavaa mtu
anayeimiliki .
“Kuna mavazi unatakiwa uvae
kidogo, mavazi ya kipapaa yale, sometimes unatakiwa uwe nayo muda wote,
kuna vitu vingi…watu wasijue kwahiyo watu washajua watu kibao kuwa mimi
nina ile, afu kuna watu wanazitafuta zile ili wafanyie mambo yao”.
Alimaliza.
Mwezi wa pili mwaka huu gazeti la Ijumaa liliandika habari isemayo ‘SOO LA BASTOLA, TUNDA MAN AKIONA CHA MOTO’.
Hiki ndicho kilichoandikwa katika gazeti hilo:
‘TABIA
ya baadhi ya mastaa kuonyeshaonyesha bastola hadharani kimemtokea puani
‘memba’ wa Kundi la Tip Top Connection, Khalid Ramadhani ‘Tunda Man’
baada ya hivi karibuni kuitwa na jeshi la polisi na kuhenyeshwa.
Akizungumza
na Ijumaa hivi karibuni Tunda Man alisema makala iliyotoka kwenye
gazeti ndugu na hili la Ijumaa Wikienda ikieleza jinsi baadhi ya wasanii
wanavyozianika silaha kiholela imemfanya akione cha moto kwani wakati
akizungumza na mwandishi wetu alikuwa Kituo cha Polisi cha Kati
(Central) akihojiwa.
“Kwanza naomba nikwambie
kuwa hakuna kitu ambacho kimenikosesha amani leo (Jumatatu) kama hii
habari yako uliyoandika kwenye gazeti, hivi ninavyoongea na wewe niko
‘sentro’ nikihojiwa, kiukweli sina amani,” alisema Tunda Man.
No comments:
Post a Comment