Rapper ROMA Amefunguka kuwa bado vituo vya
television Tanzania havijaitendea haki video yake mpya ya 2030 ndio maana
kuna mashabiki wake hawajaiona mpaka leo.
Kama kawaida kazi za Roma hupata wakati mgumu
kupenyeza kwenye radio na tv kwa sababu ya ujumbe wa nyimbo hizo. Sababu
hio imefanya kazi za Roma za Video kutazamwa zaidi kwenye mitandao
kuliko kwenye television hapa Tanzania.
Video ya 2030 imetoka 11/11/2013 na imekuwa moja ya video iliyotazamwa
sana youtube kwenye account ya Nisher ila bado 2030 haijapata muda wa
kutosha hewani kupitia tv za bongo. Kuna mashabiki wa Roma waliopo
sehemu za mbali na hawawezi kuiona kupitia youtube.
Mpaka leo video ya Roma ft Story - 2030 imetazamwa mara 21,574.
No comments:
Post a Comment