,

,

Tuesday, 26 November 2013

Nani mwanasoka bora zaidi Afrika?


Shindano la BBC la mchezaji soka bora zaidi Afrika, limerejea tena .Walioteuliwa ni watano. Nani ataibuka na ushindi na kung'aa Afrika?
Akiwa mchezaji wa zamani wa timu ya vijana ya AC MILAN, soka la Pierre Emerick Aubameyang lilianza kuchomoza baada ya kujiunga na klabu ya Saint Etienne kwa mkataba wa kudumu mnamo mwaka 2011.
Victor Moses ni mchezaji mwenye umri wa miaka 22, ambaye kwa sasa anachezea klabu yake ya nne ya Liverpool baada ya kuhama kwa mkopo kutoka klabu ya Chelsea
Akiwa mchezaji wa timu ya Chelsea ya England kwa miaka saba, John Mikel Obi amecheza mechi 187 na kushinda kombe kadhaa, likiwemo la ubingwa wa Ligi Kuu ya England
Matunda ya mwanasoka Jonarthan Pitroipa kuibuka kuwa 1 wa watakao wania tuzo ya BBC yalionekana hasa baada ya kuanza kwa michuano ya kombe la mataifa barani Afrika
Kwa wengi anajulikana na kukubalika kama mmoja wa Viungo bora katika kizazi cha sasa cha wanasoka.Yaya Toure ni roho ya Timu akitawala na kuheshimika
source BBC

No comments:

Post a Comment