Mrembo anayefanya vizuri katika mambo mengi sana
nchini Jokate Mwegelo amezungumza na kutaja Mambo manne yanayomfanya
apendwe sana na wanaume wengi hapa nchini.
1. Kujiamini
Hii
ndi sababu kubwa ya kwanza aliyoitaja jokate. Ansema hamna kitu
kinachowavutia watu, hasa wananume kama kujiamini. Mwanaume anapenda
msichana anayejiamini. Zaidi ya yote hamna kitu kinachosema kuwa “I’m sexy” Zaidi ya mwanamke anayejiamini
2. Kujitegemea
Hii
ni kama sababu ya kwanza hapo juu, Jokate anasema hamna kitu
kinachowaboa wanaume kama mwanamke ambaye anapenda vitu vya kupewa.
Ukimuonesha mwanaume wewe unapenda kutafuta vya kwako basi jua
atakupenda sana
3. Kupendeza
Jokate
anasema ni muhimu kwa wadada kuvaa nguo nzuri ambazo zitakupendeza
kulingana na mwili wako hasa hasa nguo zenye rangi ya kuonekana.
4. Tabasamu
Tabasamu kila saa kwani tabasamu linakufanya unaonekana mzuri Zaidi.
No comments:
Post a Comment