Rais Kikwete ametoa ushauri huo wakati akitoa hotuba yake kwenye
sherehe za maadhimisho ya siku ya uhuru wa Tanzania Bara, ambapo
ameelezea mengi mazuri aliyoyafanya rais wa kwanza mzalendo wa Afrika
Kusini, Nelson Mandela na kuwataka viongozi wa Tanzania kuiga mfano wa
maisha yake ikiwa ni pamoja na kusamehe na kusahau bila kulipa kisasi.

“Najua kuna wengine hapa wamepanga kulipa kisasi, wanasema nikipata
watanikoma.” Amesema rais Kikwete na kuwataka waache yaliyopita yapite
na kuendelea kuganga yajayo, “acheni kulipa kisasi.” Rais Kikwete
amesisitiza.

Hotuba ya Rais Kikwete ilijikita zaidi katika maisha ya mzee Nelson
Madiba Mandela, katika kuungana na Afrika Kusini kuomboleza kifo cha
kiongozi huyo shupavu na kutoa mfano wa jinsi viongozi wa Afrika
wanapaswa kuiga mfano wa uongozi.
No comments:
Post a Comment