Miaka ya Mapema

1952
Rolihlahla Mandela, mwanawe chifu, alizaliwa katika kijiji kimoja
kiitwacho, Mvezo katika mkoa wa Eastern Cape nchini Afrika Kusini tarehe
18 Julai mwaka 1918. Alikuwa mtu wa kwanza katika familia yake kwenda
shule. Mwalimu ambaye hata hangeweza kutaja jina lake vyema, alizoea
kumuita Nelson. Alitoroka mjini Johannesburg mwaka 1941 ili kuepuka
kulazimishwa kuoa mapema. Alikutana na Walter Sisulu aliyemsaidia kupata
kazi katika kampuni ya ya Witkin Sidelsky na Eidelma. Pia alijiunga na
chama cha (ANC)
Kesi ya Uhaini
1956
Mandela alifuzu kama wakili na kuanzisha kampuni ya kwanza ya sheria
inayomilikiwa na mtu mweusi mwaka 1952 na kuiendesha kwa ushirikiano na
Oliver Tambo, na kutoa huduma za kisheria kwa wale ambao walikosa
uwakilishi. Akihofiwa kupigwa marufuku na serikali ya ubaguzi wa rangi,
ANC ilimtaka Mandela kuhakikisha kuwa chama hicho kinaweza kuendesha
harakati zake kimya kimya. Alikamatwa mwaka 1956 na kufunguliwa mashtaka
ya uhaini yeye pamoja na wenzake 155. Baada ya kesi yake iliyochukua
miaka minne, ilitupiliwa mbali . Mnamo mwaka 1958, Mandela alimuoa
Winnie Madikizela.
Kufungwa Maisha
1964
Sheria ya hali ya hatari ilitangazwa baada ya polisi kuwaua waandamanaji
69 mjini Sharpville mwaka 1960. Serikali ilihofia kuwa wangelipiza
kisasi na hivyo kuharamisha chama cha ANC. Chama hicho baadaye
kiliendesha harakati zake za kijeshi kichinichini wakiongozwa na
Mandela.Mwaka 1962, Mandela alikamatwa kwa kosa la kuondoka nchini bila
kibali. Wanachama wengine wa ANC walikamatwa. Akiwa jela Mandela
alishtakiwa kwa kosa la hujuma. Yeye na wengine saba walihukumiwa jela
katika kisiwa cha Robben mwaka 1964
Huru hatimaye
1990
Jamii ya kimataifa iliiwekea vikwazo zaidi serikali ya ubaguzi wa rangi
nchini Afrika Kusini. Vikwazo vya kwanza viliwekwa mwaka 1967.Shinikizo
zilizaa matunda na mnamo mwaka 1990, rais FW De Klerk akakiondolea
marufuku chama cha ANC. Tarehe 11 Februari, Mandela aliachiliwa baada ya
miaka 27 jela. Umati wa watu ulimshangilia huku yeye pamoja na mkewe
wakiondoka sehemu ya jela. Katika mkutano wa kwanza wa chama cha ANC
mwaka uliofuata, Mandela alichaguliwa kama kiongozi wa chama .Mazungumzo
yakaanza ya kuunda serikali ya pamoja ya waafrika weusi na wazungu.
Tuzo ya amani ya Nobel
1993
Mnamo mwaka 1993, Mandela na rais wa nchi hiyo wakati huo, walituzwa
tuzo ya amani ya Nobel kwa juhudi za kuleta uthabiti Afrika Kusini.
Akikubali tuzo hiyo, Mandela alisema kuwa ” tutafanya kila tuwezalo
kuweza kuleta mageuzi duniani.”
Rais mpya
1994
Mnamo mwaka1994,kwa mara ya kwanza katika historia ya Afrika Kusini,
watu wa rangi zote walipiga kura katika uchaguzi huru na wa
kidemokrasia. Mandela alichaguliwa. Akihutubia umma, katika sherehe ya
kuapishwa kwake, tarehe 10 mwezi Mei, mwaka 1994, alisema: “uhuru
utawale, Mungu aibariki Afrika!” Tatizo lake kubwa lilikuwa ukosefu wa
nyumba za kutosha kwa watu maskini na mitaa ya mabanda iliendelea
kuongezeka.Thabo Mbeki alichukua uongozi wa nchi huku Mandela akiuza
sera za nchi hiyo kimataifa.
Akitoka Robbben
1995
Kuadhimisha miaka mitano baada ya kuachiliwa kwake, Nelson Mandela
alizuru kisiwa cha Robben mwezi Februari mwaka 1995 alikozuiliwa kwa
miaka 18. Ziara yake ilikuwa mwaka 1956 mwezi Februari pamoja na
wafungwa wenzake waliowahi kufungwa kisiwani humo na kufanya kazi ngumu.
Mapafu ya Mandela yanasemekana kuathirika alipokuwa anafanya kazi
katika machimbo ya mawe.
‘Usiniite”
2004
Thabo Mbeki alichukua mamlaka kutoka kwa Mandela kama kiongozi wa chama
tawala ANC na hata kushinda uchaguzi wa mwaka 1999.Mandela alimuoa Graca
Machel, mjane wa aliyekuwa rais wa Msumbiji, akiwa na miaka 80.
Aligunduliwa kuwa na saratani ya Tezi Kibofu na hivyo kuanza
matibabu.Mnamo mwaka 2004, alitangaza kujiuzulu, akisema kuwa anataka
maisha ya kimya nyumbani kwake na familia yake. Kwa mzaha aliwaambia
wandishi wa habari wasimpigie simu.
Sherehe ya siku ya kuzaliwa kwake
2008
Wanamuziki, waigizaji na wanasiasa waliungana na Mandela katika sherehe
kubwa uwanja wa Hyde Park mjini London kusherehekea miaka 90 ya kuzaliwa
kwake. Akiongea na wale waliofika, aliwaambia, ”ni wakati kwa kizazi
kipya kuchukua uongozi, kibarua kwenu sasa.”
Kuugua
2010
Mandela aliweza kuonekana hadharani mara kadhaa baada ya kustaafu.
Ingawa alionekana katika sherehe ya kukamilika kwa dimba la kombe la
dunia mwaka 2010 nchini humo. Januari mwaka 2011, alilazwa hospitalini
kwa ukaguzi maalum, huku serikali ikiwakumbusha watu kuwa aliwahi kupata
matatizo ya kupumua. Alipokea matibabu ya ugonjwa wa mapafu mwaka 2012
na pia mwaka 2013 .
Kufariki
2013
Nelson Mandela anefariki usiku wa kuamkia lea baada ya kuugua kwa muda mrefu maradhi ya mapafu.