Saturday, 16 November 2013

USAFIRI BORA WA UMMA NI SEHEMU YA MAENDELEO


USAFIRI BORA WA UMMA NI SEHEMU YA MAENDELEO
Haijalishi unatoka upande gani wa Tanzania lakini kikubwa ni kujiuliza wapi ambapo kuna maendeleo wakati usafiri wa umma haueleweki? Jibu rahisi ni hakuna hiyo sehemu si kwa Bongo tu bali popote duniani, maana usafiri wa haraka na uhakika hasa wa umma hurahisisha shughuli za kimaendeleo.

Kitendo cha mtu kuwahi kufika kazini huongeza ufanisi wa utendaji kazi na kufika nyumbani mapema huongeza ufanisi wa akili kwa mwanadamu yeyote.Kuna kila sababu ya kuboresha usafiri wetu hapa nchini ili kufika pale tunapopataka kiuchumi, kisiasa, kijamii, kitamaduni na chochote mchenye kuleta maendeleo kwa umma.
Mfano:- Daktari ni mtu muhimu sana kwa afya maana uzembe wake kidogo waweza katisha maisha ya wengi. Kazi yake inaambatana na usafi wa mwili na mavazi. Usafiri wetu wa umma bila kutoka jasho na kukubali kuchafuka haujafika kazini. Je! Daktari huyu akikataa kuchafuka ili afuate masharti ya kazi yake ni watu wangapi wataathirika kiafya na maendeleo pia?

No comments:

Post a Comment