LILE sakata la madai kwamba, staa mkubwa
wa filamu za Bongo, Jacob Stephen ‘ JB’ amenaswa akiwa na mke wa mtu
mjini Dodoma limeingia katika sura tofauti baada ya habari yenyewe kujaa
utata.
Staa mkubwa wa filamu za Bongo, Jacob Stephen ‘ JB’.
Habari za awali zilidai kuwa, tukio hilo
lilitokea wikiendi iliyopita katika hoteli moja (jina lipo) iliyopo
mjini Dodoma ambapo JB alikutwa na mke huyo wa mtu aliyetambulika kwa
jina moja la Sarah.
Kwa mujibu wa mwanaume aliyedai kuwa ni
mume wa Sarah aitwaye Rama (jina moja), alifuatilia nyendo za mkewe huyo
kwa saa kumi na mbili siku ya tukio na mawasiliano yake ambapo kwa muda
mrefu alikuwa akiwasiliana na JB ambapo walipanga kukutana katika
hoteli hiyo usiku.
Saa tatu usiku, Rama alifika ndani ya
hoteli hiyo na kuingia kwenye chumba alichokuwa amelala JB na mwanamke
huyo ambapo aligonga mlango kwa muda mrefu baadaye sana ndipo
ukafunguliwa.
Baada ya mlango kufunguliwa, kwa mujibu
wa mume wa Sarah, JB alipokea kipigo cha haja kutoka kwa mwanaume huyo
ambapo wahudumu wa hoteli na polisi waliokuwa wanafanya doria katika
shoo ya Jahazi iliyokuwa ikiendelea kwenye ukumbi wa hoteli hiyo
waliingilia kati kumuokoa JB na walipelekwa Kituo cha Polisi cha Area D
ambapo maelezo yalichukuliwa na kutakiwa warudi kesho yake.
Mwanaume huyo alisema kuwa kesho yake waliporudi polisi walimshinikiza akubali yaishe ambapo walilazimishwa kuelewana.
Mume huyo akasema hakurudi nyumbani tangu siku hiyo mpaka juzi hata hivyo akasema:
“Mimi simuhitaji tena japokuwa ana
mimba ya miezi minne na sina uhakika kama ni ya kwangu kwani tabia zake
sizielewi bora niachane naye maana tulikuwa wachumba hatujafunga ndoa.”
HUYO ALIKUWA MUME, JB SASA
Mapaparazi wetu walifanikiwa kumuweka mtu kati JB ambapo baada ya kumuuliza kilichotokea, alisema:
“Mimi nifumaniwe! Hivi inawezekana
kweli? Mna uthibitisho au ushahidi wowote? Yule msichana alikuwa klabu,
akachukua namba yangu. Si yeye tu, mashabiki wengi waliniomba namba siku
hiyo.
“Ulikuwa usiku akarudi klabu, mimi nilikuwa hotelini, akanipigia na kusema anataka kuniona ana shida ya kisanii.
“Hata alipokuja sikuwa nimefunga mlango,
akaingia na bado mlango ulikuwa wazi. Muda mfupi baadaye akaingia huyo
bwana akiwa peke yake na kusema amenifumania.
“Hivi jamani, kweli unakwenda kumfumania
mkeo upo peke yako? Kwanza hatari! Nilipoona anachachamaa kwa madai
hayo, nilitoka nje, huyo anayesema mkewe naye akaondoka lakini alikuwa
akisema mbele yake kwamba hajaolewa.
“Kule nje niliwaambia wenye hoteli,
wakaamua kuita polisi maana alikuja kunifanyia fujo. Sijui nini
kiliendelea, lakini ukweli ni kwamba sikufumaniwa.”
Sarah alipopatikana hewani juzi alisema
hajafumaniwa na huyo anayedai ni mumewe ni mpenzi wake tu. Alidai kama
kufumaniwa angekutwa akiwa hana nguo.
No comments:
Post a Comment