Irene Uwoya ameamua kuanza mazoezi ya kupunguza unene na kujiweka
fiti na kurudisha mvuto wake wa awali ambao unadaiwa kupotea mara baada
ya kujifungua huku media na wataalamu wa fashion wakimuandama mara kwa
mara kuwa kapoteza mvuto wa mwanzo kwa kujiachia kunenepeana kiasi cha
kupoteza mvuto. Owoya yupo chini ya mwalimu wake wa mazoezi Rashid
Matumla ambaye ni bondia maarufu nchini na pia wanakuja na filamu wakiwa
pamoja ambayo inaitwa Raundi Ya 8.
akizungumza na Filamucentral
“Nimejipanga kwa kufanya mazoezi ya nguvu chini ya mwalimu wangu Rashid
Matumla na nipo fiti kwa ajili ya kujifua najua kuigiza ndio ajira
yangu lakini nikijiachia na kunenepa bila mpango nitaanza kucheza nafasi
za akina bibi muda si mrefu na najiona mwili
unavyoninyemelea sitaki manyama uzembe”
Filamu hiyo imeshutiwa Tanga, Dar es salaam na Morogoro huku waigizaji wengine wakiwa ni Francis Cheka na Lumolwe Matovolwa.
Uwoya akiwa na Rashid Matumla………………..
No comments:
Post a Comment