Thursday, 28 November 2013

Wolper Ataja Idadi ya Wanaume aliowahi kuwa nao.....Wapo Diamond, Alikiba, Jux ,Dallas na Wengineo...!!


MOYO huhifadhi mengi mazito hasa ya kuumiza! Staa mkubwa wa sinema za Kibongo, Jacqueline Wolper Massawe amejikuta akimwaga machozi wakati akianika siri tano nzito kuhusu mapenzi katika mahojiano (exclusive interview) na Amani kwa takriban saa mbili.

Katika ‘intavyu’ hiyo iliyofanyika Jumatatu iliyopita kwenye Ofisi za Global Publishers, Bamaga-Mwenge jijini Dar kuanzia saa 8:44 alasiri hadi saa 10:44 jioni, Wolper alifunguka vitu vingi.

KISA/MKASA
Akizungumza kwa masikitiko, uchungu na majuto, Wolper alisema hawezi kumsahau mwanaume huyo ambaye ni Abdallah Mtoro ‘Dallas’ kwa namna alivyomwingia kijanja na kutaka kumvunjia heshima aliyoijenga karibia miaka kumi nyuma.

ALIANZIA WAPI NA DALLAS?
Siku ya kwanza Dallas alinipigia simu na kuniambia aliniona Magomeni (Dar). Naikumbuka sana siku hiyo, ilikuwa baada ya mizunguko yangu, mwanzoni sikupokea simu yake kwa sababu ilikuwa namba ngeni kwangu.


“Nilimsikiliza sana. Jamani yule mwanaume anaongea kwa ushawishi wa hali ya juu mno. Nilishangaa aliponieleza kila kitu kuhusu familia yangu na nyumbani kwetu. Kumbe tayari alishaunda urafiki na baba yangu (mzee Massawe).
“Mwanzoni nilidhani ni tapeli. Nikamkatia simu. Akaendelea kunipigia na nilipoona imekuwa kero kubwa nilipokea. Ili kuthibitisha anawajua wazazi wangu, alinitajia namba zao za simu ambazo ni za kweli.


“Pamoja na hilo nilimfanyia nyodo, si unajua mtoto wa kike? Lakini aliniongelesha kwa upole hadi nikapunguza nyodo zangu.
“Aliniuliza nataka anifungulie biashara gani. Nikamwambia biashara ya nguo. Akaniuliza nataka mtaji kiasi gani. nikamwambia dola laki moja kwa sababu nilikuwa sitaki fremu moja, nilitaka nyumba nzima. Akaniambia hakuna tatizo.
“Pia aliniuliza naishi wapi? Nikamwambia Sinza (Dar) alionesha dharau kwenye simu akaniambia atanihamishia Mbezi Beach.
“Aliniuliza natembelea gari gani? Nikamwambia Toyota Noah. Akaniambia ningependa aninunulie gari gani? Nikamjibu Toyota Discovery lakini yeye akasema ataninunulia Toyota Harrier.
“Kweli baada ya siku mbili-tatu nililetewa Toyota Harrier nyeusi nyumbani. Niliogopa isijekuwa mtego nikaingia kwenye matatizo hivyo nilimzungusha mtu aliyeniletea hadi Sinza-Mori nikamwambia apaki kwenye kituo cha teksi, nikaenda na dereva nikalichukua hadharani ili lolote likitokea nipate msaada.


“Nilikabidhiwa funguo za lile gari na documents zake, nikaondoka nalo hadi nyumbani kwangu. Kesho yake Dallas alimtuma mtu aniletee dola za Kimarekani 15,000 (zaidi ya Sh. milioni 24). Nilipouliza za nini aliniambia ni kwa ajili ya shopping ya kutembelea Harrier niachane na zile swaga za kwenye Noah (fedha inaongea). Kisha akanitumia cheni ya dhahabu.


Siku iliyofuata alinitumia Sh. milioni 15 nipeleke nyumbani nikawaambie wazazi nimepata mchumba ambaye angeenda kujitambulisha baadaye. Niliwaambia ni Dallas ambaye walikiri kumfahamu kwa sababu alishawapigia simu na kujitambulisha kuwa ni mkwe wao.”


AMESHAKUTANA NA DALLAS?
“Hadi hapo nilikuwa sijamuona Dallas kwa sura na fedha nilikuwa natumiwa kila siku.
“Wakati hayo yakiendelea akaagiza nihamishiwe Mbezi Beach na kununuliwa lile gari lililoibua mzozo BMW X6.
“Nakumbuka siku niliyokabidhiwa lile gari nililia sana. Sikuamini macho yangu kwa sababu Dallas aliniambia amenitumia kazawadi kumbe ni BMW X6 (lina stori ndefu inakuja)!


“Kumbuka mwanzoni nilikuwa na boyfriend ambaye tulipendana sana lakini hatukupanga kufunga ndoa. Nilimweleza kila kitu akakubaliana na mimi japokuwa aliumia.
“Maskini! Kuanzia hapo nikawa nimeachana na yule boyfriend wangu lakini hakukuwa na namna kwa sababu niliamini nimepata mchumba wa kunioa.


ATAKIWA KUBADILI DINI
“Baadaye Dallas aliniambia nimeshakuwa mchumba wake hivyo nibadili dini. Kweli nilibadili nikawa Muislam na jina langu likawa Ilham. Hicho kilikuwa kipindi kigumu sana maishani mwangu kwa sababu nilionekana ni muasi katika dini yangu ambayo mama ni mzee wa usharika na mwimba kwaya, baba ni mtu wa kanisani sana.”


NINI KILIFUATA?
“Siku moja nilikuwa Tanga nashuti filamu, nilikuwa nikitoka hapo niende Morogoro. Dallas alinipigia simu akaniambia yupo Nairobi (Kenya) anakuja Tanzania. Nilimwambia nipo Tanga akaniambia atanifuata kule. “Niliendelea kupiga mzigo. Zilipita saa nyingi, baadaye nikiwa na kruu yangu, Dallas alinipigia simu akaniambia ameniona. 


“Nilikataa, akaniambia namna nilivyo, nguo nilizovaa na watu niliokuwa nao, alipatia. Kumbe alikuja na Toyota Prado.
WOLPER MORO, DALLAS DAR
“Tulipomaliza kurekodi Tanga tulikwenda Morogoro, yeye aliniambia anaelekea Dar. Tulikuwa tunawasiliana. Nilipomaliza kurekodi Moro nilirejea Dar. Hapo ndipo vituko vikawa juu ya vituko.


“Niliambiwa mara kaonekana sehemu akiwa na mwanamke au wanawake. Mimi sikujali kwa sababu nilipomuuliza aliniambia hatuwezi kuonana kwa sababu kipindi hicho alikuwa katika swaumu hivyo akionana na mimi nitamharibia. (ulikuwa mwezi mtukufu).


BADO HAWAJAKUTANA?
“(Mguno) Hapo bado hatujakutana lakini yupo mjini na amejaa tele kwenye kumbi za starehe.
“Baada ya kumaliza swaumu, siku moja aliniambia anakuja nyumbani Mbezi Beach. Niliwaalika marafiki zangu tukapika vyakula, tukafanya usafi na kufukiza udi chumbani. Nilitandika mashuka meupe kitandani na kujipara kisha nikavaa ushungi kuanzia mchana nikakaa kama malkia nikimsubiri mchumba.


“Huwezi amini, hadi giza linaingia Dallas hakutia mguu. Nilipataje aibu kwa rafiki zangu waliotaka kumuona huyo mchumba? Ninyi acheni tu!
“Nilipomuuliza aliniambia alipata dharura kuna biashara alikuwa anafanya


HATIMAYE WAKUTANA LAKINI…
“Nilikasirika sana, nikasema huyu ni mchumba gani asiyetaka kuja kwangu? Nikampa muda wa siku tatu aje nyumbani na alete nguo zake zote. Kweli, siku ya tatu,  asubuhi nilimsikia mtu akiita ‘Ilham Wolper Dallas’. Nilishajua sauti yake kupitia simu hivyo nilimkaribisha na nguo zake nikaingiza ndani. Lakini cha kushangaza alikuja na pikipiki!


“Alishinda nyumbani siku hiyo maana kuna ndugu zake walikuja. Hatukufanya chochote. Dallas aliishia kunibusu shavuni kisha jioni akaondoka.
“Mjini kukawa hakukaliki. Natumiwa picha akiwa na wanawake tofautitofauti. Mmoja wa wanawake hao niliambiwa eti ana ‘ngoma’! Jamani hii dunia ina kichaa!
“Muda ukasonga, vitimbi vikawa vingi. Dallas simuoni. Muda wa kukaa kwenye ile nyumba uliisha hivyo nikahama na nikamwambia akachukue nguo zake.


UCHUMBA WAVUNJIKA, SASA ANAPUMZIKA HAPA
“Baadaye uchumba ukavunjika tena mimi ndiyo nilimwambia simtaki tena. Nilikaa muda hadi baadaye nilipopata mwanaume wangu wa sasa. Anani-control vizuri kwa sababu kanipita umri na ana busara. Tunapendana sana. Najuta kumfahamu Dallas. Siwezi kusahau tukio hilo katika maisha yangu. Dallas alicheza na hisia za moyo wangu. (akaangua kilio) Niliteseka sana. Ni Mungu tu anajua…


VIPI KURUDIA UKRISTO?
Nimekaa muda siendi kanisani. Nilikuwa najifungia ndani nalia kama mama yangu alivyokuwa anafanya. Siku moja nilimwambia mwanaume wangu akaniambia kuliko kulia kila siku bora nirudi kanisani. Ndipo nikarudia ukristo. Kwa sasa nasali Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Kijitonyama, Dar,” alisema.
MBALI NA DALLAS
Kwa mara ya kwanza Wolper alikubali kuorodhesha listi ya wanaume aliowahi kuwa nao kimapenzi kwa kuwachambua mmoja mmoja.
ALI KIBA
Bila kupepesa macho, Wolper alikiri kuwa msanii wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ndiye aliyemfundisha mapenzi: “Ni kitambo kidogo. Wote hatukuwa mastaa lakini yeye alifanikiwa kuchomoka. Kabla ya Ali (Kiba) nilikuwa na mwanaume lakini hatukuduu kwa maana ya utu uzima, ilikuwa yale ya kitoto. Lakini Ali ndiye hasa aliyeniingiza kwenye ulimwengu wa mapenzi.
KWA NINI WALIACHANA?
Ali akawa staa. Alipokwenda nje nikasikia wanawake wanamshobokea. Sasa mimi sikutaka karaha nikakaa pembeni lakini jamaa ni mtu poa sana na tukikutana tunasalimiana freshi kabisa.
DIAMOND VIPI?
“Ni kweli niliwahi kuwa na Diamond (msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul). Tulikuwa na uhusiano lakini pia alikuwa mshirika wa kibiashara (hataki kuitaja). Yeye alikuwa hawezi kulala bila kuniona, lakini tulikaa kama mwezi mmoja, kwa sasa amebaki kuwa rafiki yangu na siyo mpenzi tena kama zamani,” alisema Wolper.
VIPI KUHUSU JUX?
Jux (msanii wa Bongo Fleva, Juma Khalid) nilikuwa naye kabla ya Dallas na yule mwanaume wangu niliyeachana naye wakati wa Dallas. Katika maisha yangu nilimpenda sana Jux. Siyo marioo ni mwanaume mtafutaji aliyejiamini. Kwa sasa sipo naye. Dallas pia alichangia mimi kuachana na Jux,” alimalizia Wolper ambaye kwa sasa ana mwanaume asiyependa kumwanika.

Uanachama wa Zitto Changamoto Ndani ya CHADEMA....Wasira adai dhambi ya Ukabila Itakimaliza Chama Hicho...!!

UANACHAMA wa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Zitto Kabwe umetajwa kuwa ‘kaa la moto’ kwa uongozi wa chama hicho hata kabla ya kiongozi huyo kujibu mashitaka 11 yanayomkabili ili kunusuru uanachama wake.
 
Duru za siasa ndani ya chama hicho, zinasema Chadema haiko tayari kukabiliana na mtikisiko wa Zitto kuvuliwa uanachama, kwa kuwa hatua ya kuvuliwa madaraka tayari imegharimu umoja na utulivu wa chama hicho.
 
Taarifa hizo zinasema kwa sasa kuanzia Kamati Kuu mpaka wanachama, kuna mpasuko mkubwa ambao namna pekee ya kuuziba ni kumshawishi Zitto na Mwenyekiti Freeman Mbowe, kupatana.
 
Hata hivyo, wakati jitihada za kuwapatanisha zikiendelea, duru za siasa zinaeleza kuwa kambi ya Mbowe ina wajumbe wanaoshinikiza kumtosa Zitto na kuwa tayari kukabiliana na gharama zake.
 
Majimbo
Mtoa habari wetu kutoka ndani ya Chadema anaeleza kuwa hofu kubwa iliyopo kama Zitto atanyang’anywa uanachama, ni ukweli kuwa katika Uchaguzi Mkuu wa 2015, wanaweza kupoteza majimbo mengi na kuipa mwanya CCM kupita kirahisi.
 
“Ni kweli huu si mgogoro wa kwanza kwa Chadema na mara zote viongozi walipovuliwa madaraka kulitokea mtikisiko, lakini si kama huu wa Zitto… mbaya zaidi, majimbo ya viongozi tuliowavua madaraka leo hii yamepokwa na CCM, hatuko tayari kupoteza zaidi,” alisema mtoa habari huyo ambaye hakuwa tayari kutajwa jina.
 
Akitoa mfano, alisema mgogoro kati ya Chadema na Katibu Mkuu wa zamani Dk Aman Kabourou, ndio ulisababisha jimbo la Kigoma Mjini lililokuwa moja ya majimbo ya Chadema, leo hii kukaliwa na CCM.
 
Mbali na Kigoma Mjini, mtoa habari huyo alikumbushia pia jimbo la Tarime, alikokuwa Makamu Mwenyekiti, Chacha Wangwe, ambalo mbali na kushinda katika uchaguzi mdogo baada ya kifo chake, leo linashikiliwa na CCM.
 
“Unajua hata kwa Zitto (Kigoma Kaskazini) ukiangalia kama kweli tukimtosa, sina hakika kama tutarejesha lile jimbo. Na hata kwa Arfi (Said, Makamu Mwenyekiti aliyejiuzulu, Mbunge wa Mpanda Kati), kama yule mzee tukimchezea hatuna chetu,” alisema.
 
Alipoulizwa afafanue kuhusu mpasuko huo, alikataa na kuhoji: “Kwani wewe huoni, mbona wenzenu wameandika mpasuko uliotokea katika Kamati Kuu?”
 
Mbali na mtoa habari huyo, hata katika waraka unaodaiwa kusababisha mtafaruku huo ambao Dk Kitilla Mkumbo alikiri kuuandaa, Chadema imetajwa kuwa na udhaifu wa kushinda majimbo katika uchaguzi mdogo.
 
“Tangu uongozi huu uingie madarakani, kumefanyika uchaguzi mdogo mara nane, lakini tumeshinda mara mbili tu sawa na asilimia 25,” alisema Dk Mkumbo katika waraka wake.
 
Usuluhishi
Pamoja na Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu kutangaza kumwandikia Zitto mashitaka yake na kumpa siku 14 za kujibu, tayari kumeripotiwa kuwa nyuma ya pazia chama hicho kimeamua kumwangukia Zitto yaishe, ikiwa ni pamoja na kumwahidi cheo kikubwa kuliko Naibu Katibu Mkuu.
 
Kwa mujibu wa taarifa hizo katika uchaguzi mkuu wa Chadema Juni mwakani, Zitto atashawishiwa kugombea nafasi ya Makamu Mwenyekiti bila mpinzani au na mpinzani dhaifu na Mbowe ataachiwa kugombea uenyekiti bila mpinzani au na mpinzani dhaifu, lengo likiwa kurejesha umoja wakati wakijiandaa na Uchaguzi Mkuu wa 2015.
 
Pia inadaiwa Zitto ataahidiwa kupewa fursa ya kugombea urais wa Tanzania katika Uchaguzi Mkuu wa 2020.
 
Wasira
Akizungumzia mgogoro huo akiwa mkoani Kagera, Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Stephen Wasira, alisema anajivuna kwamba ndani ya chama chake hakuna ubaguzi kama ilivyo katika vyama vingine vya upinzani ambavyo alidai kiongozi wa ngazi ya juu lazima atoke kabila fulani.
 
Alidai katika baadhi ya vyama, ikitokea mtu ametoka kabila tofauti akataka kugombea uongozi ngazi ya juu, kunazuka vurugu na kufukuzana kwa visingizio vya kuvunja katiba za vyama hivyo.
 
“Mara nyingi huwa natumia kauli ya Mwalimu Julius Nyerere kuwa ubaguzi ni sawa na kula nyama ya mtu, ukiishaionja huiachi kwa hiyo wameionja inawatafuna. “CCM hatuna sababu ya kushangilia matatizo yao na hatuwaogopi wala hatutaki upinzani ufe, kwa sababu upinzani ni mfumo ulio ndani ya nchi, ila nasi tuache makundi yanayotokana na uchaguzi, ili tuendelee kushika Dola kama ilivyo ada yetu,” alisema Wasira.
 
Vyuo vikuu
Baadhi ya wanachama wa Chadema, wakiwamo wanafunzi wa vyuo vikuu, walikutana Dar es Salaam jana na kutangaza mgogoro wa kiutawala kati ya wapigania demokrasia ndani ya chama hicho na wahafidhina.
 
Wanachama hao waasi ambao walisema ni wapigania demokrasia ndani ya chama hicho; lakini kwa tafsiri ya viongozi wa Chadema ni ‘wahaini’, wametangaza kuzunguka nchi nzima kuhamasisha wanachama wa chama hicho wakatae baadhi ya watu waliopandikizwa kwa kukaimishwa nafasi za uenyekiti kwa manufaa ya wahafidhina.
 
Baadhi ya wanachama hao wakiongozwa na Greyson Nyakarungu, walidai wanatambua kuwa mgogoro ndani ya Chadema umetokana na Mwenyekiti Mbowe kutamani kuendelea kuongoza chama kwa gharama yoyote.
 
Nyakarungu alidai Mbowe anatamani aendelee kutawala hivyo kuzunguka katika baadhi ya mikoa na kuwaondoa katika nafasi zao viongozi waliochaguliwa kidemokrasia, ambao wanaonekana kutomwunga mkono kwa kisingizio cha kutowajibika.
 
Nyakarungu ambaye alijiita Brigedia wa Uasi huo, alisema watu wote waliopenyezwa kukaimu nafasi hizo za uongozi mikoani wajiondoe haraka “kabla hatujawaondoa kwa nguvu.
“Sisi tumeamua kama tulivyozunguka nchi nzima na kampeni ya Washa Taa Mchana, tutazunguka nchi nzima kuwaambia wanachama ubovu huu wa wahafidhina. “Tunamwonya Zitto na Dk Mkumbo tabia zao za kusema kuwa wanaheshimu uamuzi wa CC huku wakijua ni nini kitatokea, waache mara moja, kwani unyonge wa aina hii ni kuendelea kuruhusu baadhi ya watu kupora rasilimali za chama,” alidai Nyakarungu.
 
Nyakarungu, Jeremia Fumbe wa Chuo Kikuu cha Ardhi na Likapo Bakari ambaye alifukuzwa Chuo Kikuu cha Dodoma, walisema wao ni majeruhi wa kufinyangwa kwa demokrasia ndani ya chama hicho, na kila hoja ambayo wanatoa wamekuwa wanaitwa masalia ya Zitto.
 
Nyakarungu alisema watu wote wanaoitwa wasaliti ndani ya chama hicho au ‘wanaotumwa na CCM’ hoja yao imekuwa moja tu ya matumizi ya fedha za chama hicho, hoja ambayo pia walidai imemgharimu Zitto.
 
“Tunafikia hatua wahafidhina wanasema wazi kuwa ni bora chama kishuke daraja kuliko kupewa mtu wa nje, mtu wa kuja, mtu wasiyemfahamu,” alisema Nyakarungu na kusisitiza kuwa wanachama wa Chadema kutoka Mara na Kigoma ndio wamekuwa wahanga zaidi.
 
Nyakarungu, ambaye alidai alijiunga na chama hicho mwaka 2005 na kushiriki kujenga, alisema kilichomponza Zitto ndani ya chama hicho ni kuhoji matumizi ya chama hicho kupitia kamati ya Bunge ya PAC, ndio maana alishambuliwa yeye binafsi wakati huo ulikuwa uamuzi wa Kamati ya Bunge.
 
“Viongozi wetu wa Chadema wanahoji Serikali na matumizi ya fedha za walipa kodi wakitaka uwazi na usawa, leo wanataka kutonywa mapema ili wafanye marekebisho ya kuficha uovu wa matumizi ya pesa? “Zitto kama kiongozi anayejipambanua asingeweza kuwatonya ili wafiche uchafu katika matumizi ya fedha huku akitengeneza nafasi ya kuumiza vyama vingine, hii ni dalili ya udikteta. Na kwa kuwa aligusa mkia wa mfalme nge ni lazima ang’atwe,” alidai Nyakarungu.
-Habari leo

"Ray na Johari wana laana yangu na hawawezi kuiepuka"...Norah


BAADA ya hivi karibuni staa wa filamu Bongo, Ruth Suka ‘Mainda’ kueleza mazito kuhusu Ray, Johari na Chuchu Hans, msanii mwenzake, Nuru Nassoro ‘Nora’ naye amefunguka kuwa laana ya walichomfanyia miaka ya nyuma itawatesa Ray na Johari mpaka kifo chao.


Akizungumza na GPL, Nora alisema Ray na Johari walimfanyia ‘mambo mabaya’ yaliyosababisha kupotea kabisa kwenye sanaa ya filamu hadi alipoibuka upya hivi karibuni.

“Kinachowasumbua Ray na Johari ni laana yangu na kweli nimeamini Mungu analipa hapahapa duniani kwani walinifanyia mambo ya ajabu, wakanipoteza kabisa kwenye fani, walinifanya nichanganyikiwe wakijua sitapona, lakini sasa hawaelewani tena wakati walikuwa wanapendana kama pete na kidole.
 
“Nakumbuka zamani nilikuwa nikishonea nywele nzuri lazima Ray naye akamnunulia Johari kama hizo za kwangu, alimtengeneza Johari akawa anaigiza kama mimi na kujifanya yeye ndiyo mimi mpaka waliponipoteza kwenye fani.

Namshukuru Mungu nimejikongoja na hatimaye nimerudi tena kwenye sanaa, mabaya waliyokuwa wakinifanyia yamewarudia wenyewe, jamani mwacheni Mungu aitwe Mungu kwani nakesha nikiomba na ninaamini maadui zangu wote wataumbuka mchana kweupe,” alisema Nora.

Baada ya Zitto kuvuliwa Uongozi......Vijana CHADEMA wachapana makonde na kuchana Bendera ya Chama huko Jijini Mbeya...!!

Uamuzi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) wa kuwavua nafasi za uongozi vigogo wake watatu akiwamo aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe, umepokelewa vibaya na baadhi ya wafuasi wao ambao wameamua kupigana ngumi na  kuchana  bendera  za  chama  hicho.
Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, alivuliwa nyadhifa zake sambamba na aliyekuwa mjumbe wa Kamati Kuu, Dk. Mkumbo Kitila na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba.

Kamati Kuu ya chama hicho ilichukua hatua hiyo Ijumaa iliyopita, baada ya kubaini waraka wa usaliti waliouandaa ukiibua tuhuma mbalimbali dhidi ya chama na viongozi wake ngazi ya taifa.
NGUMI ZAPIGWA MBEYA
Kundi la vijana wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa Zitto jijini Mbeya wanadaiwa kuchana  bendera  za  chama  hicho  na kurushiana makonde na viongozi wa Chadema katika ofisi ya chama hicho Wilaya ya Mbeya Mjini kwa madai ya kutofautiana msimamo kuhusiana na uamuzi wa Kamati Kuu.


Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Mbeya Mjini, David Mwambigija maarufu kwa jina la ‘Mzee wa Upako’, alithibitisha kutokea kwa vurugu hizo juzi mchana.
 
Mwambigija alisema kuwa chanzo cha vurugu hizo ni vijana zaidi ya 18 wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa Zitto kuanza kufanya vikao vya siri mjini Mbeya kwa nia ya kukihujumu chama.
 
Alisema uongozi wa chama ngazi ya wilaya ulipopata taarifa hizo alizodai kuwa ni za kiintelijensia na kuwa yeye (Mwambigija) ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati Tendaji ya chama hicho wilaya, aliamua kuwaandikia barua ya kuwaita ofisini kwa lengo la kuwahoji.

Alisema vijana hao walipofika ofisini kwake huku wajumbe wa Kamati Tendaji wakiwa tayari wameketi kwa ajili ya kuwahoji, waliingia ndani ya ofisi na kulazimisha wahojiwe kwa pamoja badala ya kuhojiwa mmoja mmoja.

Alisema walipotakiwa watoke nje ili kila mmoja ahojiwe kwa wakati wake, waligoma na kukataa kutoka ofisini na ndipo yeye kama Mwenyekiti alipoamuru kikosi cha ulinzi wa chama hicho maarufu kwa jina la Red Bridged kuwatoa nje kwa nguvu na ndipo vurugu hizo zilipoanza.
 
“Ni kweli kumetokea vurugu kubwa ofisini kwetu wakati kikao cha kamati ya utendaji kikihitaji kuwahoji vijana wanaoendesha vikao vya siri kutaka kukihujumu chama kutokana na uamuzi wa Kamati Kuu kumvua Zitto madaraka, tumepata taarifa hizi kwa njia zetu za kiintelijensia kuwa vijana hawa wapo kwenye kundi la Zitto,” alisema Mwambigija.

Hata hivyo, Mwambigija alipotakiwa  kuonyesha uthibitisho juu ya tuhuma dhidi ya vijana hao, alisema kuwa ushahidi bado ni siri kwa vile wametumia njia zao za kiintelijensia kubaini mtandao wa vijana hao.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Mkoa wa Mbeya, Joseph Kasambala ambaye ni mmoja wa vijana walioitwa kuhojiwa na kamati ya utendaji alikanusha madai hayo na kusema kuwa vurugu hizo hazikuwa na uhusiano hata kidogo na  usaliti  wa  chama.

Alisema chanzo cha vurugu hizo ni Kamati hiyo kumuita na kutaka kumuhoji kinyume cha katiba ya Chadema yeye (Kasambala) ambaye ni kiongozi wa mkoa, hivyo hawezi kuhojiwa wala kuwajibishwa na kamati hiyo ambayo ni ngazi ya wilaya.

Alisema kuwa Katiba ya Chadema inaeleza wazi kuwa kingozi wa mkoa mamlaka yake ya nidhamu ni Kamati Kuu ya Chadema Taifa, hivyo kitendo cha ngazi ya wilaya kumuita na kutaka kumuhoji ni ukiukwaji wa Katiba.
 
“Mimi baada ya kupata barua ya kuitwa na Kamati hiyo ikinieleza kuwa nina tuhuma ambazo hazikuandikwa kwenye barua waliyoniletea, nilikwenda ofisini ili nipewe tuhuma zangu kwa maandishi kama ambavyo Katiba inaelekeza, lakini nikashangaa eti wanataka wanihoji, nikakataa walipotaka kunishinikiza vijana wakawajia juu wakipinga nisidhalilishwe na ndipo vurugu zile zilipoanza,” alisema Kasambala.

Walimu wachapana Makonde ofisini kwa kutuhumiana kula pesa za kisima cha shule huko Sengerema..!!

Afisa Elimu msingi wilaya ya  Sengerema Bw,Juma Mwajombe alipokuwa akimvua madaraka Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Luhama kwa kosa la kutotimiza majukumu yake. 
 
AFISA Elimu wa Shule za Msingi Sengerema Mkoani Mwanza, Bw Juma Mwajombe amemvua madaraka Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Luhama iliyoko kata ya Katwe kwa kushidwa kutekeleza majukumu yake.
 
Amesema kuwa amefikia maamuzi hayo kutokana na mwalimu huyo kushindwa kusimamia vema majukumu yake na kutokusimamia maadili ya walimu wake wanapokuwa kazini.
 
Bw, Mwajombe amemtaja aliye mvua madaraka hayo kuwa ni Mwalimu  Maila Majula baada ya kuchochea ugomvi kati ya mwalimu Emanuel  Joely  na Mwalimu Alfonsia Ndalahwa uliosababisha walimu hao kutwangana makonde ofisini  kwa kile kinachodaiwa kuwa walituhumiana kula fedha za ujenzi wa kisima cha shule hiyo.
 
Aidha amesema kuwa Mwalimu Mkuu anapaswa kusimamia vema majukumu yake na kushauri walimu kuacha migogoro isiyo ya lazima na kuzingatia maadili ya kazi na siyo kukuza migogoro isiyo ya lazima na kusababisha walimu kutokuheshimiana sehemu za kazi.

Mume Amuaa Mkewe Mjamzito wa miezi 9 kwa kumpiga mawe...Alikuwa amebakiza Siku 2 tu Ajifungue..!!

JESHI la Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, linamshikilia Philemon Ng’ambi, mkazi wa Madale Kata ya Wazo, jijini Dar es Salaam kwa tuhuma za kumuua mkewe, Enea Kagine kwa kumshambulia kwa mawe na matofali hadi kumuua.
                                                        marehemu enzi za uhai wake


                                         mama mzazi wa marehemu akilia kwa uchungu


Philemon anadaiwa kufanya unyama huo kwa marehemu mkewe aliyekuwa amebakiza siku mbili kabla ya kujivungua usiku wa kuamkia Jumamosi iliyopita  nyumbani kwake Wazo-Hill.
Akisimulia mkasa huo kwa mapaparazi wetu, jirani wa wanandoa hao aliyejitambulisha kwa jina la Fikiri Rashid alisema:
Mimi nyumba yangu na yao zinatazamana hivyo siku ya tukio majira ya saa tisa usiku, nilianza kumsikia marehemu akipiga mayowe ya kuomba msaada akisema mumewe anamuua.



Nilitoka nje kwa lengo la kutaka kutoa msaada lakini nilihofia maisha yangu hivyo ilinibidi niwaite vijana wa ulinzi shirikishi ambao baada ya muda walifika eneo la tukio na kumkuta mtuhumiwa akivunja vyombo vya ndani kama mtu aliyechanganyikiwa, wakati huo tayari alikuwa ameshamuua mkewe.
“Baada ya kuwaona ulinzi shirikishi, alikimbilia chumbani na kwenda kujificha uvunguni kwenye kitanda huku watoto wao watatu wakiwa wamelala.
 


Bila kuchelewa, askari wa ulinzi shirikishi walimkamata na kuwasiliana na Askari wa Kituo cha Polisi cha Wazo ambao walifika eneo la tukio na kumtia mbaroni mtuhumiwa pamoja na kuuchukua mwili wa marehemu kwa ajili ya taratibu za kipolisi,” alisema Fikiri.



Kufuatia tukio hilo la kusikitisha wanahabari wetu walifika katika Hospitali ya Mwananyamala ulipohifadhiwa mwili wa mwanamke huyo na mtoto wake waliyemtoa akiwa amefia tumboni.
Miili hiyo ilizikwa Jumatatu iliyopita (Novemba 25) mwaka huu katika kaburi moja kwenye Makaburi ya Madale, Dar es Salaam.

"Kama kuna wanawake wanataka kuzaa na mimi muda wowote nawakaribisha...."....Baba Kanumba


BABA wa marehemu Steven Kanumba, Charles Kusekwa amefunguka kuwa baada ya kutangaza kuwa wanawake wanaotaka uzao wake wajitokeze azae nao, wamejitokeza kumi lakini akawapa masharti, yakawashinda.

Akizungumza na mwandishi wetu, baba Kanumba aliweka bayana kuwa warembo hao waliojitokeza aliwapa sharti la kwenda kupima Ukimwi lakini ajabu wote waliingia mitini.
“Wamejitokeza vizuri lakini nashangaa wote wamekuwa wazito katika suala la kupima Ukimwi wameingia mitini, kama wapo wengine watakaolimudu sharti hilo, nawakaribisha,” alisema baba Kanumba

CHADEMA Ngoma bado Nzito...Zitto Kabwe amburuza polisi katibu wa chama hicho akimtuhumu kuusambaza waraka wa siri uliomchafua


WAKATI Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kikimwandikia Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe barua ya kumtaka ajieleze dhidi ya tuhuma zinazomkabili, yeye ameamua kukimbilia polisi akimshitaki mmoja wa viongozi wenzake.

 
Habari za kuaminika zimedai kuwa Zitto ambaye hivi karibuni alivuliwa cheo chake cha unaibu katibu mkuu wa CHADEMA, inadaiwa amefungua mashitaka polisi akimtuhumu Katibu wa CHADEMA Mkoa wa Dar es Salaam, Henry Kileo kwa madai ya kusambaza waraka katika mitandao ya kijamii.
 
Akithibitisha tukio hilo, wakili wa Kileo, Peter Kibatara, alisema kuwa mteja wake amemriwa kufika makao makuu ya Jeshi la Polisi leo Jumatano saa nane mchana na kuonana na mmoja wa maofisa wa juu wa jeshi hilo, aliyetajwa kwa jina moja tu la Mbutta, kufuatia mashitaka yaliyofunguliwa na Zitto dhidi yake.
 
Akizungumza kwa njia ya simu na mwandishi wetu, Kileo alikiri kuitwa polisi, ingawa alidai hajui ni waraka gani anaotuhumiwa kuusambaza unaomchafua Zitto.
 
“Kwa kweli sijui hata mimi ni waraka gani, ingawa hivi karibuni kulikuwa na waraka wa siri uliodaiwa kutoka CHADEMA, na ambao ulijaa tuhuma za usaliti. Lakini huo tuliishaukana siku nyingi. Labda kuna mwingine,” alisema Kileo.
 
Zitto kutwa nzima ya jana hakuweza kupatikana kwa njia ya simu kufafanua mashitaka aliyofungua polisi. Simu zake zote za kiganjani zilikuwa zimezimwa.

-Tanzania daima.

ICC yataka Kenyatta kuwepo mahakamani



Rais Uhuru Kenyatta
Mahakama ya Kimataifa ya kushughulikia kesi za uhalifu wa kivita, ICC imetengua uamuzi wake wa awali uliomruhusu Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta kutohudhuria baadhi ya vikao vya kesi ya uhalifu wa kivita inayomkabili.
Mahakama hiyo sasa imesema kuwa ni lazima Bwana Kenyatta afike binafsi mbele ya mahakama hiyo kusikiliza kesi yake na ushahidi unaotolewa dhidi yake.
Mahakama hiyo imesema kama sheria inavyotaka, Bwana Kenyatta lazima binafsi ahudhurie vikao vya kesi inayomkabili. Imesema maombi yoyote ya baadaye ya kutaka asihudhurie baadhi ya vikao vya kesi hiyo, yatafikiriwa kutoka na msingi wa suala linaloombewa ruhusa hiyo.
Mahakama hiyo imefikia uamuzi kwamba hukumu iliyotolewa katika rufaa ya tarehe 25 Oktoba 2013 ya Mwendesha mashitaka dhidi ya William Samoei Ruto na Joshua Arap Sang, imetoa taarifa mpya muhimu ambayo inahalalisha kuangaliwa upya kwa suala la kesi hiyo.
Mahakama ya Rufaa ya ICC imehitimisha kuwa Mahakama ina hiyari kwa mujibu wa kifungu namba 63(1), kinachosema kuwa "mtuhumiwa ni lazima awepo mahakamani wakati kesi inayomkabili ikiendeshwa", lakini hiyari hiyo imewekewa kikomo. Mahakama ya Rufaa imetoa uamuzi kwamba mtuhumiwa kutofika mahakamani, inaruhusiwa tu pale panapokuwa na sababu maalum na za kipekee, na lazima sababu hizo ziwe zinakidhi hoja kwa mtuhumiwa kutofika mahakamani hapo.Imeendelea kusema kwamba uamuzi wa kama mtuhumiwa aruhusiwe kutohudhuria sehemu ya vikao vya kesi yake lazima uzingatie hali halisi ya ombi la mtuhumiwa.
Fatou Bensouda, Mwendesha Mashtaka Mkuu ICC
Awali mahakama hiyo ya ICC katika uamuzi wake wa tarehe18 October 2013, ilitoa masharti kwa upande wa utetezi wa Bwana Uhuru Muigai Kenyatta kuwepo mahakamani hapo wakati wa ufunguzi na kufunga kesi inayomkabili badala ya kuwepo wakati wote. Wakati huo angeweza kusikiliza maelezo kutoka pande zote na kusikiliza maoni ya waathirika wa ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa 2007 nchini Kenya.Pia angetakiwa kuwepo siku ya kufunga kesi hiyo kwa kusikiliza hukumu yake.
Kutokana na uamuzi huo wa kumruhusu Bwana Kenyatta kuhudhuria vikao vya ufunguzi na kufunga kesi yake pamoja na vikao vingine ambavyo angeitwa pale mahakama inapoona umuhimu wa yeye kuwepo mahakamani, ulipingwa na mwendesha mashitaka tarehe 28 Oktoba 2013, kwa kukata rufaa, akitaka kuangaliwa upya kwa uamuzi wa tarehe 18 Oktoba 2013, ambapo mwendesha mashitaka aliomba mahakama kufuta uamuzi wake wa kumruhusu mtuhumiwa kutohudhuria baadhi ya vikao vya kesi yake na badala yake mahakama izingatie sheria kuu chini ya kifungu cha 63(1).
Bwana Kenyatta ameshitakiwa kama mchochezi asiye rasmi, akikabiliwa na mashitaka matano ya uhalifu dhidi ya binadamu, yakiwemo mauaji, kuhamishwa watu kwa nguvu, ubakaji, utesaji na vitendo vingine visivyo vya kibinadamu, vinavyodaiwa kufanyika wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi nchini Kenya mwaka 2007-2008. Mashitaka dhidi yake yalithibitishwa tarehe 23 Januari 2012, na kesi hiyo kukabidhiwa Chemba namba V(b) ya mahakama hiyo ya ICC. Kesi yake imepangwa kuanza kusikilizwa katika mahakama hiyo tarehe 5 Februari 2014.
source; BBC

Roma Asema Kuna Mashabiki Wake Hawajaona Video Ya 2030, Fuatilia Hapa

Rapper ROMA Amefunguka  kuwa bado vituo vya television Tanzania havijaitendea haki video yake mpya ya 2030 ndio maana kuna mashabiki wake hawajaiona mpaka leo.
Kama kawaida kazi za Roma hupata wakati mgumu kupenyeza kwenye radio na tv kwa sababu ya ujumbe wa nyimbo hizo. Sababu hio imefanya kazi za Roma za Video kutazamwa zaidi kwenye mitandao kuliko kwenye television hapa Tanzania.

Video ya 2030 imetoka 11/11/2013 na imekuwa moja ya video iliyotazamwa sana youtube kwenye account ya Nisher ila bado 2030 haijapata muda wa kutosha hewani kupitia tv za bongo. Kuna mashabiki wa Roma waliopo sehemu za mbali na hawawezi kuiona kupitia youtube.

Mpaka leo video ya Roma ft Story - 2030 imetazamwa mara 21,574.

Picha:Rais Kikwete ahudhuria kwenye semina ya kamata fursa twenzetu jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt .Jakaya Mrisho Kikwete Jana Novemba 26 alikuwa ni mgeni rasmi kwenye semina ya kamata fursa twenzetu iliyofanyika katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Mh.Rais ameupongeza uongozi wa kampuni ya Clouds Media Group kwa ubunifu wao wa kampeni hii ya fursa inayowakutanisha na kuwamasisha vijana mbalimbali nchini kujituma na kufanya kazi ili kutokomeza suala zima la ukosefu wa ajira.

Semina hiyo ilihudhuriwa pia na wasanii mbalimbali angalia picha hapa.







SHAHIRI; KITAMBI KIMENIPONZA


KITAMBI KIMENIPONZA

Kitambi kimeniponza,sina hamu asilani.
kimenifanya nawaza maisha si  ya thamani.
Mahari mara ya kwanza natakiwa milioni.
Wakashindwa kunioza kwa laki tano jamani.
Nikampenda shariza asili ya arabuni.
Ile tu kumposa dhahabu za milioni.
Ni kitambi sina pesa mi kabwela kama nini.
Kitambi kinaniponza nakosa mke jamani. 

JUX, JACK PATRICK WAKANA KUTOKA KIMAPENZI..!!

 Kwa muda mrefu muimbaji wa kundi la Wakacha, Jux na video vixen wa Tanzania, Jackie Cliff wameendelea kukanusha kuwa na uhusiano wa kimapenzi, lakini bado picha zinazowaonesha wakiwa pamoja, zimeendelea kuzalisha maswali mengi vichwani mwa watu wanaowafahamu.

Hivi karibuni, Jux alipost picha Instagram akiwa amemshikilia Jackie mkono wakitembea pamoja kama mtu na mpenzi wake na kuandika: We jus outchea livin our mfkn lives. Siku chache kabla ya picha hiyo, Jackie naye alipost picha akiwa na Jux na kuandika: My bff is better than yours..’

Miezi mitatu iliyopita , Jackie ambaye ameonekana kwenye video ya Linex ya wimbo wake Kimugina hivi karibuni, aliweka picha ya Jux na kuandika ujumbe mrefu wa kumtakia siku njema ya kuzaliwa akisema:

I don’t like to call u a friend..To me ur just a special friend..A wonderful friend..A heaven sent,And todai its your special day..God keep showering you with lots of success and blessings cuz you deserves so much more..And your so special to me..Ladies and Gentlemen help me wish Happy Bday To this handsome friend of mine
 

Msanii Steve RnB kuuaga Ukapela hivi karibuni....Amvisha Pete Mchumba wake...!!

Ni jambo la kawaida kwa wasanii wa bongoflava hasa wakubwa kama steve RnB kutembea na kila demu mzuri hapa bongo.lakini kwa steve ni tofauti kabisa kwani amefanikiwa kumvisha pete ya uchumba high school sweetheart wake.
Rumour has it kwamba steve RnB na huyu mrembo wametoka mbali na wamekuwa wapenzi wa
muda mrefu hadi wameshawahi kufukuzwa shule pamoja.tunamtakia Steve RnB safari njema ya kuelekea katika ndoa

JOKATE Atoa sababu za kwanini wanaume wengi humshobokea...!!

Mrembo anayefanya vizuri katika mambo mengi sana nchini Jokate Mwegelo amezungumza na kutaja Mambo manne yanayomfanya apendwe sana na wanaume wengi hapa nchini.

 
1. Kujiamini
Hii ndi sababu kubwa ya kwanza aliyoitaja jokate. Ansema hamna kitu kinachowavutia watu, hasa wananume kama kujiamini. Mwanaume anapenda msichana anayejiamini. Zaidi ya yote hamna kitu kinachosema kuwa “I’m sexy” Zaidi ya mwanamke anayejiamini
 
2. Kujitegemea
Hii ni kama sababu ya kwanza hapo juu,  Jokate anasema hamna kitu kinachowaboa wanaume kama mwanamke ambaye anapenda vitu vya kupewa. Ukimuonesha mwanaume wewe unapenda kutafuta vya kwako basi jua atakupenda sana
 
3. Kupendeza
Jokate anasema ni muhimu kwa wadada kuvaa nguo nzuri ambazo zitakupendeza kulingana na mwili wako hasa hasa nguo zenye rangi ya kuonekana.
 
4. Tabasamu
Tabasamu kila saa kwani tabasamu linakufanya unaonekana mzuri Zaidi.

Aibu: Mfanyabiashara maarufu jijini Dar Anaswa Live akila Uroda Gesti na Denti wa Shule ya Msingi...!!


MZEE mmoja kigogo wa biashara ya kuuza mbao jijini Dar es Salaam, hivi karibuni alinaswa kitandani ndani ya chumba akiwa na mrembo aliyedaiwa ni mwanafunzi wa shule moja ya msingi Tegeta Wazo, Dar.Mfanyabiashara huyo aliyetajwa kwa jina moja la Kyando, anasemekana amekuwa na ukaribu na denti huyo anayeitwa Fatty kwa siku nyingi, kitu ambacho kiliwapa maswali baadhi ya majirani wa nyumbani kwa msichana huyo.

Katika harakati za kuchunguza ukaribu wa msichana huyo na mtu mzima huyo, mama mdogo wa binti aligundua kuwa wawili hao wana ukaribu usiofaa.

Ikaelezwa kuwa, mama mdogo wa mwanafunzi huyo aliponyetishiwa ishu hiyo, aliandaa mtego unaofyatuka kwa kasi kuliko ule wa panya ili kumtia mikononi mzee huyo mpenda kukaa na watoto wa wenzake.

“Mtego mkali uliandaliwa, siku ya siku, ma mdogo huyo alijifanya anakwenda mbali na nyumbani, binti akaona dakika tisini za mchezo lazima aibuke kidedea wa mahaba, alimwita mwanaume huyo na kumkaribisha chumbani, kumbe arobaini zao zilikuwa zimetimia,” kilisema chanzo.

Mashuhuda wa sakata hilo walidai kuwa mama mdogo na watu wengine waliwanasa wawili hao wakiwa juu ya kitanda kama walivyozaliwa, bila kufafanua walichokuwa wakikifanya.
 

Ili kushika ushahidi mkononi, mama mdogo wa binti huyo na wapambe wake walipiga picha za mnato na za video kisha wakaanza kumuuliza maswali ‘mlalamikiwa’ ambaye inaaminika ni mume wa mtu.

Haikuelezwa wazi ni maswali ya aina gani aliyokuwa akiulizwa lakini inadaiwa yalihusu historia ya kujuana kwao.

 Aidha, inadaiwa kuwa mama mdogo huyo alitaka kumtwanga ndoa ya mkeka mfanyabiashara huyo lakini chondechonde zake nyingi zilimwokoa na kuahidi kurejea siku inayofuata kwa ajili ya kukata mshiko wa fidia baada ya kuambiwa binti huyo bado anasoma na shuleni kulilipwa fedha nyingi.

Habari nyingine zinadai kuwa wawili hao walifahamiana miezi kadhaa nyuma kupitia lifti ya gari ambayo mshitakiwa alimpa mrembo huyo maeneo ya Boko, jijini Dar.

Aibu: Angalia Picha za Utupu za Mke wa mtu Alipoliwa Uroda mara baada ya kuzidisha Pombe..!!



Mwanamke  mmoja  ambaye  ni mke  wa  mtu  na mkazi  wa  jiji  la  Mwanza  amejikuta  ndani  ya  aibu  nzito  baada ya  kulewa  pombe  na  kisha  kujipiga  za  utupu...

Habari  zinaarifu  kuwa  mwanamke  huyo  alitinga  ndani  ya  gesti  moja yenye  kaunta  ya  baa   mida  ya  mchana na  kuanza  kupata  vinywaji ( bia )

Muda mfupi baadae, mzee  mmoja  alijumuika  na  mama  huyo  na  kuendelea  kutandika  bia  mpaka  ilipopanda  utosini....

Baada  ya  kulewa  kupita  kiasi, wawili hao walijisogeza ndani  ya  chumba  kimoja  cha  gesti  hiyo  na kuanza  kusaliti  ndoa  yake  huku akijifotoa  akiwa  mtupu.... Picha  hizo  zilinaswa  na  mumewe  baadae  kupitia  simu  yake.


Tuesday, 26 November 2013

Kocha Keshi hatishiki kamwe!


Timu ya soka ya Nigeria
Kocha wa timu ya taifa ya Nigeria Stephen Keshi , anasisitiza kuwa hana wasiwasi wowote kwamba anaweza kufutwa kazi kabla ya kombe la dunia la Brazil la mwaka wa 2014.
Chini ya uongozi wa Keshi, Nigeria ilifanikiwa kufika fainali ya mwaka ujao baada ya kushinda Ethiopia 4-1 katika mechi za kufuzu kushiriki mchuano huo.
Ingawa Keshi aliyekuwa nahodha wa hapo awali wa Super Eagels, amekosa mechi mara mbili baada ya kampeni ya timu hiyo kufuzu kwa michuano hio.
Mwaka wa 2002 Keshi alikua msaidizi wa Shuaibu Amodu wakati Nigeria ilifuzu kucheza kombe la dunia, lakini wawili hao walifutwa kazi na nafasi yao kuchukuliwa na Adegboye Onigbinde kabla ya mechi za mwisho zilizochezwa Korea Kusini na Japan.
Miaka minne baadaye Keshi pia alifutwa kazi na Togo kabla ya kombe la dunia la 2006 nchini Ujerumani, ingawa alikuwa ameiongoza timu kwa mara ya kwanza hadi sasa katika historia ya nchi hio.
Hivyo basi Keshi akawa na wasiwasi kua kilichotendeka hapo awali kingejirudia kwa mara nyingine, lakini Keshi mwenye umri wa miaka 51 ana mtizamo wake wa kipekee kuhusu hali ya mchezo wa kandanda.
"kazi hii ni ya kuajiri na kufuta," Keshi alilielezea BBC michezo. "nilipofutwa kazi mwaka wa 2002 nilipata mshtuko lakini hiyo ni hali ya maisha, kwa hivyo hatuwezi kujuta na kuishi kwa machungu na masikitiko.
"tunaongea kuhusu Nigeria kwa hivyo huwezi jua kitakacho tendeka.
"lakini cha muhimu sasa hivi ni kuwa tunatazamia tu yale yajayo ambayo ni kuandaa wachezaji wangu pekee.''
"huezi jisikitisha na yaliyofanyika ama yanayoweza fanyika. Tumefaulu zaidi ya matarajio ya watu kadhaa, zoezi la kujijenga linaendelea.
"siishi na hofu ya kufutwa kazi. Kwa kusema kweli hiyo ni kumaliza tu nguvu.
Keshi alikuwa na uhusiano mgumu na waajiri wake wa shirikisho la soka la Nigeria tangu kuongoza kikosi ambacho hakikuwa na ujuzi kushiriki na kushinda kombe la taifa bingwa Afrika, kwenye mchuano uliofanyika nchini Afrika Kusini mwanzoni mwa mwaka 2013
SOURCE. BBC SWAHILI

Nani mwanasoka bora zaidi Afrika?


Shindano la BBC la mchezaji soka bora zaidi Afrika, limerejea tena .Walioteuliwa ni watano. Nani ataibuka na ushindi na kung'aa Afrika?
Akiwa mchezaji wa zamani wa timu ya vijana ya AC MILAN, soka la Pierre Emerick Aubameyang lilianza kuchomoza baada ya kujiunga na klabu ya Saint Etienne kwa mkataba wa kudumu mnamo mwaka 2011.
Victor Moses ni mchezaji mwenye umri wa miaka 22, ambaye kwa sasa anachezea klabu yake ya nne ya Liverpool baada ya kuhama kwa mkopo kutoka klabu ya Chelsea
Akiwa mchezaji wa timu ya Chelsea ya England kwa miaka saba, John Mikel Obi amecheza mechi 187 na kushinda kombe kadhaa, likiwemo la ubingwa wa Ligi Kuu ya England
Matunda ya mwanasoka Jonarthan Pitroipa kuibuka kuwa 1 wa watakao wania tuzo ya BBC yalionekana hasa baada ya kuanza kwa michuano ya kombe la mataifa barani Afrika
Kwa wengi anajulikana na kukubalika kama mmoja wa Viungo bora katika kizazi cha sasa cha wanasoka.Yaya Toure ni roho ya Timu akitawala na kuheshimika
source BBC

Ufaransa yaongeza majeshi Afrika ya Kati




Majeshi ya Ufaransa yakiwa ndani ya Kifaru cha kijeshi
Wizara ya Ulinzi ya Ufaransa imethibitisha kuwa imetuma mamia ya wanajeshi wa ziada kwenda kusaidia kuimairisha hali ya usalama Jamuhuri ya Afrika ya Kati.
Maafisa ya Umoja wa Mataifa umesema hali ya usalama nchini humo ni ya wasi wasi huku ikionya huenda mauaji ya halaiki yanaweza kuendelea.
Ufaransa imekuwa ikitoa msukumo kwa azimio la Baraza la Umoja wa Mataifa ambalo linazungumzia namna ya kuyasaidia majeshi ya kulinda amani ya Umoja wa Afrika.
Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Jan Eliasson amesema raia katika eneo la Jamuhuri ya Afrika ya Kati wamekuwa wakikumbana na matatizo yaliyozidi uwezo wao ikiwa ni pamoja na unyanyasi wa kijinsia, utesaji, mauaji na fujo kati ya wakristo na waislamu.
Majeshi ya Umoja wa Mataifa yamekuwa yakijaribu kuimarisha hali ya usalama nchini Afrika ya Kati tangu Rais Francois Bozize apinduliwa mwezi Marchi.